Forklift ikiwa kazini
                                                           Na Dotto Mwaibale
BOHARI
 ya Dawa (MSD) imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na 
kushusha (Forklifts) sita, zenye gharama ya shilingi za kitanzania 
milion 531. 8, ambazo zimetolewa msaada na Mfuko wa Kimataifa wa Global 
Fund kupitia Shirika la Marekanila Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).
Msaada
 huo ni sehemu ya awamu ya pili ya maboresho ya maeneo ya kuhifadhia 
dawa ya MSD yaliyokuwa ya kifanywa na Global Fund, ikiwa ni pamoja na 
upanuzi wa maghala ya kisasa yaani WiB ya MSD Makao makuu, Dodoma na 
Mbeya, na ujenzi wa maghala ya Kisasa MSD Kanda ya Tabora na Kituo cha 
mauzoTanga.
Wakizungumza
 katika makabidhiano hayo, yaliyofanyikaa jana katika utekelezaji wa 
awamu ya mwisho ya upanuzi na ujenzi wa maghala ya kisasa yanayojulikana
 kama Warehouse in -a –box, mashine hizo (forklifts), Naibu Mkurugenzi 
Mkazi wa JSI/SCMS Marasi Mwencha amesema fedha hizo ni zile zilizosalia 
kutoka kwenye ujenzi wa maghala ya kisasaya MSD, ambapo walikubaliana na
 menejimentiya MSD kununulia forklift.
Mkurugenzi
 Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amewashukuru wahisani hao kwa mashine 
hizo ambazo ni za gharama, na kueleza kuwa mashine hizo zitapelekwa 
kwenye kanda za MSD zenye uhitaji.
Hata
 hivyo ameeleza kuwa tayari MSD ina Kiwanja maeneo ya Luguruni, wilayani
 Ubungo jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kujenga ofisi na ghala la 
kisasa kwa Kanda ya Dar es Salaam hivyo wanategemea kuendelea 
kushirikiana na wahisani kwa ajili ya ujenzi pindi taratibu 
zitakapokamilika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni