Pichani ni Mpendwa wetu Jennifer Livigha maarufu aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la CHINGA ONE na Mwanachama mwanzilishi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake Kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiliki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.
Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer
Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama
Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu
Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer
Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'
Baadhi ya ndugu wa karibu, Jamaa na Marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu Jennifer
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo
Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi
Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu
Baadhi ya ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea
Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.
Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer
Safari ya kuelekea Nachingwea ikiwa imeanza .Picha zote na Fredy Njeje wa TBN
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Msingi ya Mogitu wilayani Hanang baada ya kuzindua madarasa ya shule hiyo, Februari 21, 2017. Watatu kulia ni Mbunge wa Hanang, Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAIBU WAZIRI MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA GENERALI MPYA WA IDARA YA UHAMIAJI NCHINI, DK. ANNA MAKAKALA
posted on
Serikali ya India inayoongozwa na Kashmir imepiga marufuku harusi za gharama kubwa katika eneo hilo.
Sherehe ya upande wa bibi harusi hairuhusiwi kualika watu zaidi ya 500, na kwa upande wa bwana harusi sherehe yao hairuhusiwi kualika watu zaidi ya 400.
Serikali ya Kashmir pia imesema mlo katika harusi haupaswi kuzidi vyakula vya aina saba, ili kuhakikisha kuwa hakuna chakula kinachopotezwa.
Aidha, mbunge mmoja anapanga kuwasilisha pendekezo kama hilo ili kudhibiti harusi za gharama kubwa katika nchi yote ya nchini India.
Wakazi wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamekumbwa na hofu ya kuwa huenda wamekuwa wakilishwa nyama ya punda baada ya kuonekana mabaki ya vichwa vya punda katika maeneo kadhaa ya kaunti hiyo.
Mkazi wa kaunti ya Kirinyaga katika kijiji cha Murubara Bi, Wariara Githinji amesema wameshangazwa kubaini vichwa vinne vya punda vikiwa vimetelekezwa katika eneo mabalo wanyama hao wamechinjwa.
Vichwa hivyo na mabaki mengine ya punda ikiwemo utombo vilibanika na watoto waliokuwa wakienda shule ambao walikuwa wakishangaa hali iliyowavuta watu wazima waliokuwa wakipita njia.
Baadhi ya watumishi wa serikali na Halmashauri za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)