SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

w1
Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
w2 
Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.
w3
Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
w5
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.
w6
Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam .Kulia nia Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma. (Picha na frank Mvungi- Maelezo)

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI,JIJINI DAR ES SALAAM LEO

mp1 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
mp2
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
mp3
Wadau wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
mp4Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MKURUGENZI WA AMANA BANK AFUNGUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA TAWI LA MWANZA



 
Benki ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo <b>Dk Muhsin Masoud alitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama ioneshavyo pichani.

Mkurugenzi huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini &nbsp;hapo ili kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini.

Kilele hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na Main, vile vile Arusha na Mwanza.

WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AZINDUA UNUNUIZI WA HISA ZA BENKI YA WALIMU - MCB

tr1 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akigonga kengelle kuashiria uzinduzi wa ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tr2
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua uuzaji wa hisa za Benki ya Walimu MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam, uliofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tr4
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo uliyofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tr5
Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majlaiwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuzindua mpango wa Benki ya Walimu MCB – MCB kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es salaam Novemba 27, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dares salaam.3065 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

EALA ENACTS FOREST MANAGEMENT BILL

Hon Christophe Bazivamo, mover of the Bill on Forestry Management and Protection Bill, 2015.

The Secretary General, Amb Richard Sezibera (left) and the Minister for EAC Affairs, Rwanda, Hon Valentine Rugwabiza in discussions at the Plenary sitting yesterday
Hon Judith Pareno presented the Report of the Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources. 

EALA has passed the EAC Forests Management and Protection Bill 2015 in effect putting in place a regional framework to conserve the environment.

The Bill whose mover is Hon Christophe Bazivamo sailed through at its 3rd Reading after the Committee stage scrutinized its various clauses, proposing amendments. The Report of the Agriculture, Tourism and Natural Resources was presented by Hon Judith Pareno on behalf of the Chair.

The EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015 hopes, to promote the development, protection, conservation, sustainable management and use of the forests in the Community especially trans-boundary forests ecosystems, in the interest of present and future generations. It further wants to espouse the scientific, cultural and socio-economic values of forests and harmonise national forest laws.

Once amends are integrated, the Bill is expected to undergo assent by the Heads of State in line with Article 63 of the Treaty for the Establishment of EAC.The Bill seeks to operationalize Article 112 (1) d) of the Treaty for the Establishment of the EAC in which Partner States undertook to co-operate in the management of the environment and agreed to take necessary disaster preparedness, management, protection and mitigation measures especially for the control of natural and man-made disasters.

The Bill delineates the roles and responsibilities of Partner States and seeks to promote uniformity and integration in the area of Disaster Risk Reduction (DRR) and management.Finally, the Bill seeks to create a regional mechanism which would enable a timely intervention in disaster situations.

The Assembly had at its last sitting in Nairobi in October 2015, adjourned debate on the Bill. The adjournment at Committee stage followed the successful Motion for the same, tabled by the Chair of EAC Council of Ministers, Hon Dr Harrison Mwakyembe, seeking for more time to enable the United Republic of Tanzania to make input.

Hon Dr Mwakyembe then informed the House that the United Republic of Tanzania was expected to go to the polls in October and that it was necessary for the debate to be put on hold until such time that a new Government is in place to effectively enable the Partner State to make its input.

The Bill has five parts with the Preliminaries and objectives contained in Part 1. Part two covers general measures on forest management and protection while Governance and institutions of forest management and control are entailed in part 3 of the Bill. Part 4 amplifies trade in forest related products while section 5 envisages co-ordination matters under a Board known as the EAC Forests Board to be operationalized by the Council of Ministers.

ASKARI WA HIFADHI NI MARUFUKU KUPIGA RAIA;-TANAPA

Meneja uhusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Pascal Shelutete akisisitiza jambo wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake,picha na maktaba ya manyara leo blog

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, AMOS MAKALLA ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA NYUMBA YA MUNGU NA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA SAME - MWANGA - KOROGWE

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akipewa maelezo wakati akikagua kituo cha kufua Umeme bwawa la Nyumba ya Mungu
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akikagua ujenzi mradi wa maji wa Same- Mwanga- Korogwe

DAR ES SALAAM TO HOST 16 TH EAC JUA KALI-NGUVU KAZI EXHIBITION

The 16th edition of the East African Community Jua Kali/Nguvu Kazi Exhibition will take place from 30th November to 6th December, 2015, at the Mnazi Mmoja Grounds in Dar es Salaam, Tanzania. The theme of the Exhibition is Buy Micro and Small Enterprises (MSEs) products, Build East Africa.

According to the EAC Principal Trade Officer (Internal) Mr. Nduati Wa Karanja, the theme portrays the role MSEs are expected to play in the growth and development of the region’s economies. Mr. Karanja disclosed that so far 1,000 artisans had registered and confirmed their participation. The distribution of artisans who have so far confirmed participation according to the as follows: - Burundi, 50; Kenya, 250; Rwanda, 100; Uganda, 80, and; the host United Republic of Tanzania, 520.

The 16th EAC Jua Kali/Nguvu Exhibition will be officially opened on 2nd December, 2015.To participate in the Exhibition, exhibitors from Tanzania, Burundi, Rwanda and Uganda are required to register with the respective ministries of Trade and Industry, while those in Kenya must register with the Small and Medium Enterprises Authority.

In order to support promotion of the Jua Kali/Nguvu Kazi sector of the regional economy, the EAC Secretariat in collaboration with the Partner States and Confederation of Informal Sector Organization East Africa (CISO-EA) has organized the annual exhibitions since 1999. The exhibitions have proved to be strategic avenues for promoting the sector’s products, transfer of technologies, and promotion of the regional integration process.

WENGI WAJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Maelfu wajitokeza katika maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, hapa wakiendelea na matembezi ya kupinga ukatili wa Kijinsia
  Maandamano yakipokelewa na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID Daniel Moore, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Maire Matthews, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake
Lucy Melele, Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo
barani Afrika – WiLDAF, Dr. Judith Odunga, pamoja na wawakilishi wa mashirika wahisani na viongozi mbalimbali.
 Dr. Judith Odunga kutoka WiLDAF akiwakaribisha wageni.

HATIMA YA MWILI WA MAWAZO KUAGWA AMA KUTOAGWA JIJINI MWANZA KUJULIKANA LEO

                                           Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeahirisha kesi ya madai ya kuomba ridhaa ya kufanya ibada ya Mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Geita Marehemu Alphonce Mawazo iliyowasilishwa na Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi
wa marehemu Mawazo.
 

Katika kesi hiyo, mlalamikaji anaiomba mahakama kuondoa zuio la jeshi la polisi Mkoani Mwanza la kutoruhusu shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo kufanyika Jijini Mwanza, kabla ya kwenda kuzikwa Mkoani Geita.

John Mallya ambae ni miongoni mwa Mawakili watatu wa Chadema ambao wanaitetea kesi hiyo, amebainisha kuwa Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo majira ya saa saba mchana, ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha anatarajiwa kutoa maamuzi yake baada ya leo kusikiliza utetezi wa pande zote mbili zinazohusika.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema bara Salum Mwalimu, amewasihi wanafamilia pamoja na wafuasi wa chama hicho kuendelea kuwa watulivu, wakati maamuzi ya mahakama hiyo yakisubiriwa ambapo ameeleza kuridhika na mwenendo wa kesi hiyo.

Nje ya Mahakama, ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi ambapo kulikuwa na polisi pamoja na mbwa ambapo baada ya kesi hiyo kuahirishwa, umati mkubwa wa wananchi uliokuwa umetanda mita chache kutoka Mahakamani hapo ulianza kuimba nyimbo za maombolezo na kuwasindikiza viongozi mbalimbali wa chedema hadi katika hoteli waliyofikia.

John Mallya ambae ni mmoja wa Mawakili wa Chadema akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Katibu Mkuu Msaidizi Chadema bara, Salum Mwalimu akizungumza baada ya kesi kuahirishwa

PAPA FRANCIS AWASILI NCHINI KENYA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo jioni.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewasili jijini Nairobi nchini Kenya leo jioni tayari kwa ziara ya siku tatu nchini humo.

Alipotua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ( JKIA ), kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani alilalkiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.

Ziara ya Papa Francis nchini Kenya ni mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika itakayomchukua pia hadi nchini Uganda na baadaye Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. OTHMAN CHANDE ATOA SOMO KWA WAANDISHI WA HABARI.

MO1
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akitoa ufafanuzi kwa wanabari (hawapo pichani) kuhusu uandishi bora wa habari za Mahakama wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es salaam.
MO2
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (kushoto) na Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa (kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Mahakama yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
MO3
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
MO4
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam.

MATUMIZI YA TEHAMA YABORESHA UFANISI SERIKALINI

KA1
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) ambapo kikao kimoja kitawaunganisha pamoja washiriki kutoka Mikoa 8 ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja (interactivity) kwa maswali na ufafanuzi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa.
KA2
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.
KA3
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano ambapo mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) utatumika ili kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za Serikali.
KA4
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu faida za kutumia TEHAMA ikiwemo kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika awali kuandaa mikutano hiyo ambapo kwa sasa washiriki watashiriki mikutano hiyo wakiwa katika vituo vyao vya kazi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

                                                                            (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
 

                                                                            Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Uanzishaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini utaboresha na kuongeza ufanisi wenye tija ambao utapunguza gharama za utendaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kupitia utaratibu huu wa vikao kazi ambavyo vitaendeshwa kwa kutumia mfumo wa mawasiliano ya video ambapo kikao kimoja kitaunganisha kwa pamoja washiriki kutoka mikoa nane ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja kwa maswali na ufafanuzi.
 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kupunguza gharama za uendeshaji vikao kazi.

BALOZI MUSHY AMUAGA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI

Moja ya zawadi alizopokea kutoka kwa Balozi Mushy ni Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyo patikana hapa nchin.

Pia katika mazungumzo yao, Balozi Mushy alimpongeza Dkt. Gulaid kwa kuiwakilisha vyema UNICEF hapa nchini. kwa Upande wa Dkt. Gulaid naye alitumia fursa ya kumshukuru Balozi Mushy kwa niaba ya Wizara &nbsp;na Serikali kwa ujumla kwa Ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chote cha uwakilishi wa UNICEF hapa nchini.
Picha na Reginald Philip