MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AAPISHWA JANA

Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi kabla Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kushoto) wakati wa kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia hati ya kiapo kabla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo aliyomteuwa,hafla ya kiapo ilifanyika  Ikulu Mjini Zanzibar(kushoto) Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar wa mambo mbali mbali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi akielekea sehemu ya kula kiapo kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumuapisha rasmi  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Mwanasheria Mkuu wa zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto) akiwa na Viongozi waliohudhuria kuapishwa kwake ,(wa pili kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kumuapisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]

DK BENDERA ATOA MAAGIZO YA MADAWATI



 Na Mahmoud Ahmad,Manyara
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amewaagiza viongozi wa Wilaya za mkoa huo, kuhakikisha hadi mwisho wa mwezi Aprili kusiwepo na wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati ya kukalia.

Akizungumza  mjini Babati, Dk Bendera alisema japokuwa Rais John Magufuli amewaagiza wakuu wote wa mikoa kuondoa tatizo la ukosefu wa madawati  hadi Juni 30 mwaka huu, kwa Manyara mwisho ni Aprili 30.

Alisema Manyara haipaswi kusubiri hadi mwezi  Juni 30 ili imalize upungufu wa madawati hivyo, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri, viongozi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha hilo linafanyika.

“Rais wetu Dk Magufuli baada ya kututeua hivi karibuni alituagiza wakuu wote wa mikoa kuhakikisha tunamaliza tatizo hilo hadi mwezi wa sita lakini mimi nataka kwangu Manyara ikifika mwezi wanne tumalize,” alisema Dk Bendera.

Kwa upande wake, katibu tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kiwango cha elimu Manyara kimeporomoka kwa kuchangiwa zaidi na tabia ya wafugaji kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kufuata malisho mazuri ya mifugo yao.

“Hali ni mbaya kwenye halmashauri zetu zenye wafugaji wengi kwani mkoa wetu umeendelea kuporomoka kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na sekondari hivyo jitihada za dhati za kupambana na hili zinahitajika,” alisema Maswi.

Hata hivyo, aliwataka viongozi wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha shule zote za sekondari ambazo hazijamaliza ujenzi wa vyumba vya maabara, wanamaliza haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wapate elimu kwa njia ya vitendo.

UVUVI HARAMU VICTORIA TISHIO KWA UHIFADHI



Swala wapatikanao kwenye hifadhi ya Saanane kama walivykutwa na kamera ya matukio ya manyara leo jijini mwanza hivi karibuni

Na  Mahmoud Ahmad alivyotembelea ,Mwanza .

Uvuvi haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua ukitishia uhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo zimepewa jukumu la kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye uso wa dunia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya ziara ya kutembelea hifadhi hiyo ya Saa Nane   iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto inayowakabili ni uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa na wavuvi wanaojipatia kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya samaki . 
Askari Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce  Mong`ee   amesema kuwa wamekua wakiimarisha doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za uvuvi ambazo ni tishio kwa uhifadhi.
“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi mazalia ya samaki” Alisema Askari huyo
Mhifadhi huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni asilimia 90% ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Alisema Hifadhi ya Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji hivyo kuvutia watanzania wengi kutembelea  eneo hilo ambali lina wanyama pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri na maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.

WASHINDI MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO YALIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI

Mfanyabiashara Davis Mosha akiwa na mshindi wa kwanza katika mashindano ya Mbio za magari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi,Gurjit Dhan (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Shameer Yusuf (kulia).
Mshindi wa pili katika mbio za magari ,Piero Canobbio (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Silvia Frigo.
Mshindi wa tatu katika mashindano hayo Gurpa Sandhu (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Davie Sihoka.
Mshiriki wa Mbiio za magari kutoka Morogoro Bob Taylor akipokea kikombe baada ya kumaliza akiwa katika top ten.
Zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa washiriki wa mashindano hayo ya Vaisakh Rally ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro.
Mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa mbio hizo.
Zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa washindi pamoja na waandaaji.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya mbio za magari ,Gurjit Dhan (Kulia) akizungumza jambo na mshindi wa pili wa mbio hizo Piero Canobbio kutoka nchini Kenya.
Baadhi ya magari yaliyoshiriki mbio hizo.
Mashabiki wakiwa katika eneo mojawapo wakifuatilia mbio hizo.
Moja ya gari la mashindano kikivutwa mata baada ya kupata hitilafu.
Baadhi ya magari yakiwa katika mbio hizo.
Magari mengine yalilazimika kutembea bila ya gurudumu baada ya kupata hitilafu.
Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Aloo akiwa na Mwenyekiti wa matukio wa klabu ya Kilimanjaro Motorspot ,Juma Shaaban.
Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Alooakizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani ) kuhusu maandalizi ya Mbio za Vaisakh Rally 2016 zinazofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA.
 
Mkuu wa Usalama wa Kampuni ya Security Group (SGA) Absolom Jailo akizungumza namna ambavyo kampuni hiyo imejipanga kuimarisha ulinzi katika mshindano hayo.
Mkuu wa Huduma ya Kwanza katika mashindano hayo Dkt Akshay Prataap akieleza namna walivyojipanga kutoa huduma ya kwanza endapo kutatokea tatizo kwa madereva wanaoshiriki mbio hizo.
Zawadi kwa washindi.
Hari Singh Rally Team ni moja ya madereva walioingiza gari mpya aina ya Subaru za mwaka 2015 katika mashindano hayo.