SADIFA AWAPONGEZA VIJANA KWA MSHIKAMANO ARUISHA

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa UVCCM taifa, Sadifa Juma Khamisi, amewapongeza vijana mkoani Arusha kwa mshikamano walionao katika kipindi hiki cha kampeni na mshikamano ambao unatoa imani kubwa kwa chama cha mapinduzi kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Sadifa,ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Arusha kwa pamoja na baraza la UVCCM wilaya ya Arusha kilichofanyika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi mkoa.

Sadifa,amewataka vijana wasilale bali waimarishe kampeni katik kipindi hiki ili chama cha mapinduzi kipate ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao..

Amwataka makatibu wa UVCCM,mkoa na wilaya zote nchini kufanyia kazi kwa haraka pindi wanapopata taarifa za kuwepo matukio ya kuwakwamisha vijana kufanya kazi ikiwemo,kufanyiwa vurugu na  kushambuliwa na wanachama wa upinzani .

 Amewataka vijana kujipanga tayari kuwakabiri wanachama wa vyama vya upinzania ambao wanakusudia kuvuruga uchaguzi na kuwakumbusha kuwa vijana ndio walinzi wa chama cha mapinduzi.

Pia amewataka kufanya kampeni za kistaarabu ambazo zitawashawishi wapiga kura kukipigia chama cha mapinduzi kura na hivyo kuibuka na ushindi wa kishindo ila yeyote atakaye mchokoza mmoja wenu uvumilivu sio silaha ya vijana bali mjibu mapigo.

"Najua wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaharibu uchaguzi nyie muwe wastaarabu katika kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi kuanzia kwa dkta Magufuli hadi kwa madiwani wetu ifikapo oktoba 25"alisema Sadifa

Aidha mkutano huo wa ndani wa vijana jijini hapa uliofanyika katika ukumbi wa ccm mkoa uliibua hisia mbali mbali huku vijana wakitunishiana misuli hali iliyopelekea mwenyekiti huyo wa uvccm taifa kuweka sawa hali hiyo na mwisho kuondoka ukumbini hapa.

Sadifa alisema kuwa hali ya sasa ya kisiasa inavyoonekana wenzetu wamejipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa si wa amani lakini msiwafuate hadi pale watakapowachokoza ndiyo hapo vijana onyesheni kuwa nanyi ni vijana.


Mazishi ya Waziri KOMBANI Huko MOROGORO!

 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Kombani.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Celina Kombani. Nyuma yake ni Samia Suluhu.
Mama Salma Kikwete naye akiweka udongo kwenye kaburi la Kombani.
Bwana Hemed Saleh Pongoleni ambaye ni mume wa marehemu akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Celina Kombani.
Watoto wa marehemu wakiwa na mashada ya maua wakati wa maziko ya mama yao.
Viongozi mbalimbali wakishiriki maziko hayo.



Jeneza lenye mwili wa marehemu Celina Kombani likiingizwa kaburini.
Jeneza likiombewa kabla ya kuingizwa kaburini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa Waziri Celina Kombani katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiaga mwili wa Waziri Kombani leo.
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Celina Kombani kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA ZAIDI YA MARA NNE WAKATI AKIWA SAFARINI KUTOKEA JIJINI TANGA KUELEKA DAR

 Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao  wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga  Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga .