Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea
taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo,
Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa
Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji
Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa
ya makabidhiano. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu)
akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa
anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo,
kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam
leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano
ofisini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili
kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo,
Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara
baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati)
kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa
Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya
Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio
lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wa pili kushoto)
akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara
hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
SOBER HOUSE YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPIGA VITA MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA KULEVYA.
posted on
Mkuu
Wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi
(hawapo pichani) katika siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi
Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kulia ni Mkuu wa Kituo
cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji.
Mkuu
Wa Kituo cha Life and Hope Bagamoyo Sober House, Al-Kareem Bhanji aki
akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye siku ya
Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa
wa Pwani kushoto ni Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga.
Wananchi
wakifatilia mada mbalimbali kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita
Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
Waathirika wa Dawa za Kulevya akiandamana siku ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
Maandamano yakeendelea.
Kikundi cha Sana cha Bagamoyo wakiigiza kama Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga akiwa kwenye picha ya Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Kituo cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji akiwa kwenye picha ya Waathirika wa Dawa za Kulevya
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Kituo
cha Usaidizi Wa Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope
Bagamoyo Sober House leo,June 26,2016 kimeadhimisha siku ya Kimataifa ya
Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya.
Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka June 26 lakini kwa Mwaka huu Kituo cha Sober kimeadhimisha siku hiyo Wilayani Bagamoyo.
Akizungumza
katika Maadhimisho hayo,Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed
Mwanga amesema vita vya Mapambano ya Dawa za Kulevya si vya Serikali
pekee wala vya mtu mmoja bali ni vita vya kila mtu,ambaye anapaswa
kuwajibika katika eneo husika ili kutokomeza kabisa uingizwaji Wa Dawa
hizo.
Pia,Mkuu
huyo Wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi Wa Dini ,Wananchi pamoja na
Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa pamoja katika kutoa
taarifa za kuwafichua waingizaji Wa Dawa hizo ili Serikali kuwachukulia
hatua kali za kisheria.
Amesema,Serikali
imeahidi kupatikana kwa eneo kubwa ili kuendeleza kituo hicho na
kuwasaidia vijana ambao ndio waathirika wakubwa Wa janga hilo na kuitaka
jamii kuwatambua na kuwabaini waathirika wa Dawa hizo.
Kwa
upande wake,Mkuu Wa Kituo hicho cha Life and Hope Bagamoyo Sober
House,Al-Kareem Bhanji amesema kituo hicho kimesaidia watu zaidi ya 100
mpaka sasa,ambapo ametoa Changamoto za ukosefu wa Majengo kituoni hapo
jambo ambalo limepelekea kwa sasa kulipa kodi kubwa ya pango.
Pia
ameiomba Serikali kupatikana Ardhi ya kutosha ili kuweza kuongeza
majengo na kukidhi haja ya kupokea Waathirika 200 ikiwa Wanaume 150 na
Wanawake 50.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akimuonesha Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye baadhi ya wachezaji
wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys
waliopatiakana kupitia michuano ya Airtel Rising Stars wakati wa
uzinduzi wa awamu ya sita ya michuano hiyo uliofanyika Dar es Salaam
Jumapili Juni 26 2016.
Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipinga mpira
kuashiria uzinduzi wa rasmi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016.
Uzinduzi huo umefanyika Jumapili 26 Juni 2016 kwenye makao makuu ya
Airtel Tanzania Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo
wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016 jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
Waziri
wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa katika picha
ya pamoja na viongezi wa TFF pamoja na Airtel Mara baada ya uzinduzi wa
Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars
Wafanyakazi
wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari,
Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu
wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars.
Airtel yazindua msimu wa 6 wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016
Dar es
Salaam, Jumapili 26 Juni 2016 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua msimu wa sita wa mashindano
ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars na
kuwapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Serikali pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini
(TFF) za kukuza mchezo wa soka.
“Programu
za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale
duniani. Ndiyo maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising
Stars ambayo matunda yake yameonekana dhahiri katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita”, alisema Nnauye.
Alitoa
mfano wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti
Boys ambayo wachezaji wake 10 wa kutumainiwa wametokana na Airtel Rising
Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars vilevile yanaoneka dhahiri
kwenye timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo wachezaji wake wote
wanatokana na programu hii ya vijana”, alisema Nnauye. Klabu za daraja
la kwanza na ligi kuu Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya Airtel
Risings Stars.
Waziri
amewataka viongozi wa soka kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel Rising
Stars ili kuweza kubaini vipaji vingi zaidi kupitia mashindano haya ya
vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu za wasichana na wavulana
kuanzia ngazi ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya Taifa jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa kampuni ya Airtel
Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo
imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo
huo marufu hapa nchini.
Alisema
Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya
Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana
kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel
Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana
kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano
cha kipato cha kuaminika”, alisema.
“Kwa
kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar, Airtel
Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia
mchezo wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa
Tanzania. Ni njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga
mkono”, alisema.
Kwa
upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya Airtel Rising
Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa soka
hapa nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono.
Naamini kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.
Airtel
Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa
itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke,
Arusha, Lindi na Zanzibar.
Jiwe
la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na
Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa
gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiteta jambo na
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa kili kulia) akifurahia
jambo na Naibu wake (kulia), IGP,Ernest Mangu, wapili kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimia na Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli akisalimia na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi wa Utawala wa Benki ya CRDB, Beatus Segeja akisalimiana na Rais Dk. John Magufuli
Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther Kitoka akisalimiana na Rais Dk. John Magufuli.
Rais John Magufuli akizindua rasmi Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Dar es Salaam.
Rais Magufuli akipata maelezo ya namna kituo hicho kinavyofanyakazi.
Rais Magufuli akipata maelezo ya namna kituo hicho kinavyofanyakazi.
Wakurugenizi wa Benki ya CRDB wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake.
Rais John Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei baada ya kutoa hotuba yake.
Rais
John Magufuli akifurahia jambo wakati akimkabidhi Tuzo ya Ufadhili
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, wakati
wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi, uliofanyika
katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
ambapo benki hiyo imetoa zaidi ya shs. milioni 300. Kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
Rais John Magufulia (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikli. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)