Mwenyekiti
wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo
Tanzania (Chawaumiviata), Hilal Said wakati akizungumza na waandishi wa
habari katika maadhimisho ya Siku ya Mtindio wa Ubongo Duniani
yaliyoadhimishwa viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Mzazi
mwenye mtoto mwenye changamoto ya maradhi hayo, Titus Chengula
akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo.
Mzazi
Ester Peter kutoka Makuburi eneo la Ubungo akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu changamoto walizonazo kuwalea watoto wenye matatizo hayo.
Wanachama
wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo
Tanzania (Chawaumiviata), wakiwa na viongozi wao kwenye Maadhimisho ya
Siku ya Mtindio wa Ubongo Duniani yaliyofanyika hapa nchini kitaifa
viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Mama akimsaidia mtoto wake kutembea katika maadhimisho hayo.
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja.
Burudani zikiendelea.
Picha zikipigwa na mmoja wa wafadhili wao
Na Dotto Mwaibale
WAKUU
wa Shule mbalimbali wametakiwa kuwapokea watoto wenye mtindio wa ubongo
kujiunga na darasa la kwanza badala ya kuwakataa kwa maelezo shule zao
hazina walimu maalumu wa kuwafundisha.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa
Mtindio wa Ubongo Tanzania (Chawaumiviata), Hilal Said wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Mtindio
wa Ubongo Duniani yaliyoadhimishwa viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es
Salaam jana.
"Changamoto
kubwa waliyonayo watoto wenye utindio wa ubongo hapa nchini ni
kukataliwa na wakuu wa shule mbalimbali pale wanapokwenda kuandikishwa
darasa la kwanza kwa madai ya shule hizo kutokuwa na walimu wa
kuwafundisha" alisema Said.
Said alisema walimu hao wanapaswa kuwapokea watoto hao badala ya kuwakataa jambo litakalo wafanya wajione hawanyanyapaliwi.
Alisema
baadhi ya walimu wamekuwa wakiwaeleza wazazi wao kuwa wawapeleke watoto
hao katika shule maalumu zenye walimu ambazo pia haziwasaidii watoto
hao kwa kuwa wakiwa katika shule hizo wanakuwa ni watoto wenye matatizo
yanyofanana.
Said
alisema kuwachanganyanga watoto hao na watoto wengine katika shule za
kawaida inawasaidia kuwachangamsha na kujiona kama walivyo wenzao.
Mmoja
wa wazazi wa mtoto mwenye matatizo hayo Ester Peter kutoka Makuburi eneo
la Ubungo alisema maadhimisho kama hayo yamekuwa yakiwakutanisha wazazi
na watoto wao wenye matatizo hayo ambapo ubadilishana mawazo ya namna
ya kuwalea watoto hao na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.
Mzazi
mwingine Titus Chengula kutoka Ubungo External alisema wazazi wenye
watoto wenye matatizo ya afya wasiwafungie ndani badala yake wawasaidi
na kuwapekeka shule na vituo vinavyo wasaidia katika mazoezi ya viungo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni