Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la
msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square Dar es Salaam jana.
Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
CRDB, Dk.Charles Kimei, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi.
Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC), wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la
mradi wa Jengo la Morocco Square.
Rais
Jakaya Kikwete (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC), Zakhia Meghji (kulia) na Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo
na Makazi, William Lukuvi wakipiga makofi kumpongeza Rais Kikwete katika
siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika sanjari na hafla hiyo ya uwekaji wa
jiwe la msingi la jengo hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Zakhia Meghji (wa pili kulia), akimkabidhi zawadi ya sherehe yake ya kuzaliwa. |
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifungua shampeni kumpongeza Rais Kikwete katika siku yake hiyo ya kuzaliwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu,
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia),
wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo. Kushoto
ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiteta
jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela
Kairuki wakati wa hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wadau mbalimbali na Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Rais Jakaya Kikkwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wa NHC.
Na Dotto Mwaibale
RAIS
Jakaya Kikwete amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), chini ya
Mkurugenzi wake Nehemia Mchechu kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Moroco
Square ambao utagharimu sh.bilioni 150 za kitanzania hadi kukamilika
kwake.
Mradi
wa ujenzi huo utakamilika mwaka 2017 na jengo litakuwa na mita za mraba
110,000 na ukiwa na majengo manne.Mawili ni kwa ajili ya ofisi , moja
hoteli na nyingine nyumba za makazi ya watu 100, ghorofa 20 na kiwanha
cha ambapo mawili ni kwa ajili ya ofisi, moja Hoteli na lingine ni kwa
ajili ya nyumba za makazi ya watu 100 , ghorofa 20 lenye eneo la kiwanja
cha ndege kwa juu yake.
Akizungumza
Dar es salaam jana, wakati wa uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa eneo
hilo jana, Rais Kikwete alisema mradi huo ni mkubwa kuliko yote katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na utaifikisha nchi katika hatua
nyingine za kimaendeleo.
Aliongeza kuwa ni mambo mapya kuanzishwa Tanzania tofauti na siku za nyuma, hivyo alilipongeza NHC kwa kwenda na wakati.
Rais
Kikwete alisema utakapokamilika mradi wa eneo hilo la Mororco Square
utakuwa na faida nyingi kama kupunguza gharama za wananchi kwenda mijini
kutokana na huduma zote za kijamii kupatikana eneo hilo.
Alitoa
mwito kwa NHC kufungua huduma ya Online ili watu wasipate shida wawe
wanafanya kila kitu kupitia mitandao badala ya kuhangaika barabara
kwenda kutafuta huduma na matokeo yake wanapoteza muda.
Alisema
katika kuhakikisha huduma zinafanyika kwa urahisi inabidi ziwekwe
barabara za juu ili watu wanaopita katika eneo hilo wavuke salama.
"Pale
Morocco kuna njia nne, hivyo kinachotakiwa ni kuweka barabara ya juu
lakini sijui kama itawezekana kutokana na kuwa namaliza muda wangu,
lakini nawaahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za NHC,
hivyo changamoto zenu zitatatuliwa "alisema.
Kwa
upande wake, Mchechu alifafanua eneo hilo litakuwa na viwanja vya
michezo kwa watoto, maduka hivyo ni kitovu cha kuchangamsha mji kutokana
na kuwa lipo katikati ya mji.
Mwenyekiti
wa Bodi ya shirika hilo, Zakhia Meghji alisema anaamini kuwa Rais ajaye
ni Dk.John Magufuli, hivyo anaamini ataendeleza mradi huo aliouacha
Kikwete.
Alisema
umefika wakati wa kutungwa sheria itakayowezesha wageni kununua nyumba
hizo kutokana na iliyopo hairuhusu ili kupanua soko kwa wateja.
Mradi huo umefanikiwa kwa kupata mkopo wa fedha kutoka Benki ya CRDB chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu, Dk. Charles Kimei.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni