Makamu
wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal, akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani
kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard
Membe (Mb) kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw.
Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko
nchini India.
Makamu wa Rais akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Makamu wa Rais akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa akisaini
kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) kumpa
pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe
aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.
Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Mama Salma akiwapa pole familia ya marehemu.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akisaini
kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.),
kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius
Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.
Dkt. Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa Waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, akiwapa pole familia ya marehemu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.),
akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu kaka yake, Simon Membe.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Bw. Omar Mahita naye akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
Balozi wa Tanzania nchini DRC - Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -, Balozi Anthony Cheche akitoa heshima zake za mwisho .
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa Waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, akitoa heshima zake
za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Joachim Utaru, akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nigel Msangi,akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb),
akiwaongoza waombolezaji kuingia kanisani, tayari kwa Misa ya kumuombea
Marehemu.
Baadhi
ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wakiwa wamesimama
wakati mwili wa Marehemu unaingizwa kanisani, St. Peters jijini Dar es
Salaam.
Mwili wa Marehemu ukiingizwa kanisani.
Misa ikiendelea.
Kiongozi wa Misa akiendelea na Maombezi kwa Marehemu.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea
Muongozaji wa shughuli, Richard Kasesela akiendelea na matangazo.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, akitoa salamu za rambirambi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi
wa Zimbabwe hapa nchini Mhe. Edzai Chimonyo, akitoa salamu za
rambirambi kwa niaba ya Mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini.
Mapadri walioongoza misa hiyo.
Mwakilishi wa Familia ya Marehemu akitoa neno la shukrani.
Balozi
wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini na mkuu wa Mabalozi
wote wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Juma Khalifan Mpango,
akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angela Kairuki akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu.
Mwili
wa Marehemu ukiingizwa kwenye gari,tayari kwa safari ya kwenda kijijini
kwa Marehemu Rondo, Mkoani Lindi tayari kwa mazishi yanayotarajiwa
kufanyika kesho Jumatano, tarehe 07.10.2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni