Mkutano wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo endelevu barani Afrika waanza leo Victoria Falls-Zimbabwe


 
DSC_4474
Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Mh. Emmerson Mnangagwa  akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa tano wa  Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo endelevu barani Afrika  unaoendelea muda huu Victoria Falls-Zimbabwe. Ambapo amezitaka nchi za Afrika kuendelea kushikamana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukuaji wa uchumi. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)
DSC_4488
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo endelevu barani Afrika unaoendelea muda huu Victoria Falls-Zimbabwe wakifuatilia mada mbalimbali kwa watoa mada (hawapo pichani). Mada mbalimbali za kujadili juu ya Afrika hatua ya kuchukua kuelekea mkutano mkubwa wa Dunia wa COP 21, utakaofanyika nchini Paris, Ufaransa mwishoni mwa mwaka huu. 
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[VICTORIA FALLS-ZIMBABWE] Mkutano mkubwa  wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo endelevu barani Afrika umeanza rasmi leo katika mji wa Kitalii wa Victoria Falls, Nchini hapa huku ukishirikisha watu mbalimbali kutoka nchi za Afrika na nje ya Afrika.
Washiriki wanaoshiriki mkutano huu unaondelea hapa ni pamoja na wadau wa mambo ya mazingira, wanaharakati, taasisi binafsi, Serikali, Mashirika ya kijamii, Wafanyabiashara, wanahabari na viongozi wa Kiserikali na wanasiasa katika kujadili kwa pamoja.
Mkutano huo umeanza rasmi leo Oktoba 28-30, wiki hii umeandaliwa  kwa ushirikiano wa mashirika mbalimbali ikiwemo UNECA, Serikali ya Zimbabwe pamoja na mashirika mengineyo.
DSC_4482
DSC_4478
DSC_4490
DSC_4424
DSC_4434
DSC_4485
 

Msimamizi wa uchaguzi wa EU ataka vyama vya siasa nchini kuwa na dhamira ya kuimarisha demokrasia

 
 
xuttynyfcf5zwtk562fe7176465a
Muangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Sargentini, Mbunge wa Bunge la Ulaya akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) nchini.Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
 
Tanzania – Uchaguzi Mkuu 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Date: 27/10/2015
Ya kutolewa mara moja
Uchaguzi uliyokuwa na ushindani mkubwa, uliyopangwa vyema kwa kiasi kikubwa,
lakini ambao haukuwa na jitihada za kutosha za uwazi toka kwa watendaji wa uchaguzi
Dar es Salaam, 27 Oktoba 2015
Uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba ulikuwa na ushindani mkubwa, kwa kiasi kikubwa
umeendeshwa vizuri, japokuwa jitihada pungufu za uwazi zilimaanisha kuwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hazikupewa imani kamili ya vyama
vyote.
Akitoa tamko la awali la ujumbe wa waangalizi Jijini Dar es Salaam, Muangalizi Mkuu wa EU
EOM, Judith Sargentini, Mbunge wa Bunge la Ulaya, alisema japokuwa NEC na ZEC walikuwa
wamejiandaa vyema katika mpangilio wa uchaguzi, kutokuwepo kwa uwazi pamoja na
maelezo kwa wakati kuhusu daftari la wapiga kura, maelezo ya mipaka ya majimbo na mfumo
wa kurusha matokeo kumesababisha kuwepo kwa hisia hasi na kuathiri imani ya vyama juu
ya mchakato wa uchaguzi.
Siku ya uchaguzi ilionekana kuendeshwa vyema. Waangalizi wa EU walifuatilia taratibu za
upigaji kura kwenye vituo 625 katika mikoa yote nchini. Uendeshaji wa upigaji kura
ulionekana kwenda vyema katika asilimia 96 ya vituo vya kupiga kura vilivyoangaliwa na EU
EOM, kwa Tanzania bara na Zanzibar. Wawakilishi wa vyama vya siasa walikuwepo kwenye
karibia vituo vyote vilivyoangaliwa, jambo ambalo lilichangia kuwepo kwa uwazi na imani juu
ya mchakato wa upigaji kura. Tathmini ya jumla ya ufungaji pamoja na utaratibu wa kuhesabu
pia ilionekana kuwa nzuri au nzuri sana katika vituo vilivyo vingi vilivyoangaliwa.
“EU ilikuwa na waangalizi 141 kwenye mikoa yote ya Tanzania siku ya uchaguzi,” alisema Bi
Sargentini. “Japokuwa kulikuwa na matatizo madogo madogo kwenye vituo vichache vya
kupiga kura, kilichoonekana kwa ujumla ni mamilioni ya watu wakitumia haki yao ya kupiga
kura katika mazingira ya amani, na wakionyesha dhamira yao ya kuunga mkono mchakato wa
kidemokrasia.”
Bi Sargentini alisema kuwa waangalizi wa EU walihudhuria zaidi ya shughuli 139 za kampeni
nchini kote. Pamoja na mabishano kadhaa kati ya mashabiki wa vyama vinavyopingana,
baadhi ambayo kwa kusikitisha yaliishia kwa vurugu, alisema kuwa, kwa ujumla, kampeni
zilikuwa safi na za kusisimua.
Kuhusu mifumo ya kisheria, EU EOM imesema kuwa, pamoja na kuwa mifumo inayotawala
chaguzi kwa Muungano na Zanzibar inatoa msingi mzuri wa uendeshaji wa chaguzi za
kidemokrasia, kuna maswala kadhaa ambayo hayajafanyiwa kazi toka uchaguzi uliyopita.
Haya ni pamoja na kutoruhusiwa kikatiba kwa wagombea binafsi na kutokuweza kupinga
matokeo ya uchaguzi wa rais, ambayo hayaendani na misimamo ya kimataifa kwa chaguzi za
kidemokrasia.
EU EOM iliangalia vituo vya habari 16 wakati wa kampeni. Ili baini kuwa vyombo vya habari
vya dola havikutoa nafasi sawa na za haki za habari za kampeni, huku CCM ikipewa nafasi
zaidi. Hata hivyo katika mtazamo chanya, Bi Sargentini alisema kuwa baadhi ya vyombo vya
habari binafsi vilionekana kwa kiasi kikubwa kutoa uwiano.
Waangalizi wa EU watabaki nchini kufuatilia mchakato wa uorodheshwaji na utangazaji wa
matokeo, na malalamiko na rufaa zinazoweza kujitokeza.
“EU EOM itabaki nchini hadi tarehe 15 Novemba, na itakutana na vyama, maafisa uchaguzi na
asasi za kiraia,” alisema Bi Sargentini. “Kwa ajili ya wapiga kura wote waliyopanga foleni kwa
subira Jumapili, natumai ya kuwa wahusika wote wataendelea kufanya kazi ili kuwa na
chaguzi za amani, shirikishi na zenye uwazi.”
“Hitimisho la amani la uchaguzi pamoja na dhamira ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi
vitahakikisha historia ya kujivunia ya Tanzania ya uongozi, kikanda na barani,” alisema Ines
Ayala Sender, Mkuu wa Wawakilishi wa Bunge la Ulaya, ambao walijiunga na Ujumbe wa
Waangalizi wa EU siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. “Hivyo basi, nawahimiza Watanzania
wote kuwekea mkazo maisha ya kisiasa shirikishi, ujengaji imani na uaminifu, na uimarishaji
zaidi wa taasisi zinazo unga mkono demokrasia.”
EU EOM ndiyo ujumbe mkubwa kabisa wa waangalizi wa kimataifa uliyopo nchini na ambao
upo Tanzania kwa muda mrefu zaidi. Ilitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi
ulifuata ahadi za kimataifa na za kikanda kuhusiana na chaguzi, pamoja na sheria za Tanzania.
EU EOM itatoa tamko kamili lenye maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na mapendekezo kwa
chaguzi zijazo, katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya kukamilika kwa mchakato wa
uchaguzi.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Sarah Fradgley, Afisa Habari EU EOM Simu ya mkononi: +255 786 440768 Barua pepe: sarah.fradgley@eueomtanzania.eu
Tovuti: www.eueom.eu/tanzania2015 Facebook: www.facebook.com/eueomtanzania2015 Twitter: @EUEOMTanzania

Bookstore-Themed Tokyo Hotel Has 1,700 Books And Sleeping Shelves Next To Them


 
Some people love books, while other get put to sleep by them. Book and Bed Tokyo, a bookstore-themed hotel located on the seventh floor of a high-rise in Tokyo’s Ikebukuro neighborhood that opens its doors on November 5th, is perfect for both. Designed by Makoto Tanijiri and Ai Yoshida of Suppose Design Office, it promises to be the best place to curl up with a good book and fall asleep.
The ‘Compact’ compartment measures 205 x 85 centimeters (80.7 x 33.5 inches), and the ‘Standard’ is 205 x 129 centimeters (80.7 x 50.8 inches); the price per evening can be 3,800 to 6,000 yen (US$32 to $50), depending on the size of accommodations. On opening day, there will be 1,700 English and Japanese language books available, but the hotel plans to eventually expand its library to 3,000.
Traveling bookworms will soon have a new place to stay in Tokyo.
library-hotel-book-bed-tokyo-8
The Book and Bed has 1,700 English and Japanese Language books.
library-hotel-book-bed-tokyo-7
Bookshelf-beds provide an interesting place to sleep.
library-hotel-book-bed-tokyo-4
The compartments are small, but the price is right for such a prime location!
library-hotel-book-bed-tokyo-6
library-hotel-book-bed-tokyo-5
Eventually, there will be over 3000 books.
library-hotel-book-bed-tokyo-2
Book and Bed Tokyo opens its doors on November 5th.
library-hotel-book-bed-tokyo-1

TULINDE AMANI YETU TUNAPOPOKEA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU


 
Ndugu watanzania wenzetu, tunapenda kuwapongeza kwa kumaliza mchakato wa kampeni za vyama vya siasa na wagombea  kwa amani na utulivu. Vile vile tunawapongeza kwa kupiga kura kwa kwa amani na utulivu, kwani pamoja na kujitokeza kwa wingi tulipiga kura kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ukiachilia mbali kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo.
Ndugu watanzania wenzetu,  tangu juzi jumapili 25 Oktoba tulianza kupokea matokeo. Hiyo ni hatua muhimu sana kwa taifa letu, demokrasia yetu na amani ya nchi yetu. Wote tutakubaliana kwamba nchi nyingi za kiafrika zimeingia katika machafuko ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hizo katika kipindi cha kupokea matokeo.
Nchi za Ivory Cost iliingia katika mgogoro wa kisiasa kwa wakati wa kupokea matokeo, ikaingia katika mapigano  ya wenyewe kwa wenyewe maelfu ya wananchi walipoteza maisha, wengine wakijeruhiwa vibaya na wengi wakiyakimbia makazi yao.
Mwaka 2007, Nchi jirani ya kenya nayo ilingia katika mgogoro wa kupokea matokeo na hivyo kusababisha machafuko, watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha, wengi wakiachwa walemavu na maelfu wakiyakimbia makazi yao.
Sisi Global Peace Foundation Tanzania, tunaona mwenendo wa kupokea matokeo ukianza kuingia dosari, kwa baadhi ya wagombea na wafuasi wa wagombea kujitangazia matokeo. Ambao kwa Mujibu ka sheria ya uchaguzi ni kinyume, ni kuvunja kanuni kwani chombo chenye dhamana ya kutangaza matokeo ni Tume ya Taifa ya uchaguzi pekee.
Kwa sababu hiyo, tumeona tuwakumbushe wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa kuwa wakati huu wanapaswa kuwa watulivu na waangalifu pindi wanapotoa matamko. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia wafuasi wao kuwa watulivu na hatimaye kutuvusha katika hatua hii tukiwa na amani na utulivu.
Tunaisihi tume ya uchaguzi ya Taifa NEC, na ile ya Zanzibar ZEC, kuharakisha mchakato wa kutangaza matokeo pindi yanapopatikana na kujumlishwa ili kuepusha minong’ono na hisia hasi zinazoweza kupandikizwa kwa wapiga kura na wananchi na baadaye kusababisha machafuko.
Tunakiri kuwa pamoja na kuwapo migogoro ya hapa na pale, kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo kama huko Unguja Zanzibar, baadhi ya maeneo ya Mbeya, Dar es Salaam na Lindi. Bado jeshi la polisi limeendelea kufanya kazi zake kwa weledi. Hata hivyo tunakisii chombo hicho kuwa waangalifu zaidi katika kipindi hiki adhimu kwani matumizi ya nguvu zilizopitiliza yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani.
Tunawakumbusha watanzania wenzetu mashabiki wa vyama vya siasa , wapiga kura na vyama vya siasa wajiandae kupokea matokeo ya aina yeyote. kwani misingi ya kidemokrasia inatutaka kuchagua na yule aliyepata kura nyingi ndiyo anakuwa mshindi.
Na mwisho ni kwa wanahabari na vyombo vya habari nyie mnabeba dhamana kubwa kwa taifa hili katika wakati huu muhimu kwa taifa letu. Namna mtakavyotoa taarifa kwa watanzania ndiyo itakayo amua mustakabali wa amani na utulivu wa taifa hili.
Mnalo jukumu na wajibu mahususi katika kuhakikisha kuwa nchi hii inabaki salama, inabaki na umoja na mshikamano, inabaki na utulivu. Toeni habari kwa kulingana na matakwa ya taaluma yenu muhimu.
Waswahili husema, sindano ya daktari huponya na kuua na kalamu ya mwandishi hujenga ama kubomoa. Kama ilivyo daktari mwema, mwenye maadili huchagua kuponya na mwandishi makini atachagua kujenga jamii yenye amani, utulivu na mshikamano kwa kutambua kuwa bila amani hakuna maendeleo.
Tunasimamia msemo wa watanzania uliopata umaarufu katika wakati huu wa uchaguzi kuwa KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI . Asanteni, Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.
Tafadhali bonyeza hapa chini kusikiliza wimbo maalumu wa kuhamasisha Amani ulioimbwa na Barnaba Boy.

Route launch today: Harare to Victoria Falls


ae41d820-ce28-4670-9307-fdac36f49253



Harare to Victoria Falls flights start today! 

 
At 2pm CAT today we’ll take off from Harare and fly to the stunning Victoria Falls for the first time!
Tickets are on sale now for this new route, and until 30th November prices start from just Tsh 83,600 one way, including tax (Tsh 44,000 fare, plus Tsh 33,000 taxes and Tsh 6,600 VAT).
Why not combine your trip to Harare with a visit to the beautiful Victoria Falls?

UKAWA watoa tamko la kutokubaliana na matokeo ya Urais yanayotolewa na NEC


Edward-Lowassa-1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Ifuatayo ni taarifa aliyoisoma masaa machache yaliyopita katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Ndugu waandishi wa habari;
Tumewaita hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini.
Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi.
Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa.
Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.”
Ndugu waandishi wa habari;
Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
Hata hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.
Aidha, katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.
Hali kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au wameibuka washindi.
Upo ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.
Ikumbukwe kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo mbalimbali.
Ndugu waandishi wa habari;
Tunaamini kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
Wakati tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.
Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.
Ndugu waandishi wa habari;
Kutokana na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.
Ndugu wana habari
Kile kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

BILIONEA JAMES PACKER AMEFUNGUA CASINO LA KIFAHARI MACAU

Bilionea James Packer amefungua jengo jipya ya kifahari la dola bilioni 3.2 la Casino lijulikanalo kama Studio City huko Macau.

Casino hiyo imefunguliwa kwa msaada wa nyota wa filamu ya A-Listers Robert De Niro, Leonardo DiCaprio pamoja na Martin Scorsese.

Pia mpezi wa Packer mwanamuziki Mariah Carey alikuwepo ufunguzi wa jengo hilo la kifahari lenye vyumba 1,600 likiwa na bwawa la kuogelea. 
                               Muonekano wa bwawa la kuogelea katika jengo hilo la casino
 

ZEC YAFUTA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR

Taarifa zilizotufikia kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufutwa kwa uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mpaka hapo itakapotangazwa tena. 
Sababu hasa za kufutwa kwa uchaguzi huo, kunaelezewa kuwa ni kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza. 
Tamko la kufutwa kwa uchaguzi huo limetolewa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alipoongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita huko Zanzibar. 
Na hii ni taarifa kamili iliyosomwa kwa waandishi wa habari na Mwenyeikiti huyo.

ANGELINA JOLIE LICHA YA KUWA MIONGONI MWA NYOTA MKUBWA HATAKI MATANUZI

Nyota wa filamu Angelina Jolie licha ya kuwa miongoni mwa nyota wakubwa kabisa duniani lakini anapenda kuishi maisha ya kawaida badala ya yale ya udiva.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 40, ameonekana akiwasili katika uwanja wa ndege wa LAX akivuta mwenywe begi lake la matairi bila ya kuwa na msaidizi kama wafanyavyo mastaa wengine, akiwa na watoto wake.

Angelina Jolie alikuwa na watoto wake hao Maddox, Pax, Zahara pamoja na Shiloh, ambao nao walikuwa wamebeba mabegi yao mgongoni.

MAREHEMU PAUL WALKER AINGIZA FEDHA NYINGI LICHA YA KUTOKUWEPO DUNIANI

Nyota wa filamu ya Fast & Furious marehemu Paul Walker ameingia katika orodha ya jarida la Forbes ya mastaa waliokufa wanaoingiza fedha nyingi.

Walker, aliyekufa kwa ajali ya gari mwaka 2013, ameingiza dola milioni 10.5, katika mwaka uliopita na anashika nafasi ya tisa.

Mfalme wa Pop marehemu Michael Jackson anashika nafasi ya kwanza kwa mwaka watatu mfululizo, akiingiza dola milioni 115, ikiwa ni pungufu na mapato ya mwaka jana milioni 140 mwaka 2014.

Marehemu Elvis Presley anashika nafasi ya tatu kwa mastaa waliokufa lakini bado wanaingiza fedha kwa kupata dola milioni 55.

UJUMBE KUTOKA NCHI ZA MAZIWA MAKUU WAMTEMBELEA KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, VIJANA , UTAMADUNI NA MICHEZO

JA1 
Katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maziwa makuu ambao upo nchini ukiangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa Tanzania.Wengine kwenye picha ni Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya katika wizara ya mambo ya nje,Muburi Muita(wa kwanza Kushoto waliokaa) na Nancy kaizilege wa Umoja wa mataifa Tanzania.(wa kwanza kulia waliokaa).

JA2 
Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya katika wizara ya mambo ya nje,Muburi Muita(aliyenyoosha mikono) akiongea na Katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati alipomtembelea ofisini kwake na ujumbe wa kutoka eneo la maziwa makuu(ICGLR) waliokuja kuangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa Tanzania na kuelezea kufurahishwa na ushiriki wa vijana wengi katika uchaguzi huu na kwamba uchaguzi ulikuwa wa Amani na mafanikio makubwa.Ujumbe huo unajumuisha nchi za Zambia,Burundi,Kenya,Congo,Uganda na Sudan

TAARIFA KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

MAALIM SEIF APINGA UAMUZI WA MWENYEKITI WA ZEC KUFUTA UCHAGUZI WA ZANZIBAR

Na: Hassan Hamad (OMKR)
 

Chama Cha Wananchi CUF kimetangaza kutoutambua uamuzi uliotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bw. Jecha Salim Jecha, wa kuufuta uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi huu.
 

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Chama hicho Mtendeni mjini Zanzibar, mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Mwenyekiti peke yake hana mamlaka ya kufuta uchaguzi, kwa vile hakuwashirikisha makamishna wa Tume hiyo, na kuuchukulia uamuzi huo kama ni wake binafsi.
 

Hivyo ameiomba Serikali kuiachia Tume ya Uchaguzi iendelee na kazi yake ya uhakiki wa matokeo ya uchaguzi na halafu kumtangaza aliyeshinda.
 

Amesema tayari uhakiki wa matokeo ya uchaguzi wa majimbo yote 36 ya Unguja na majimbo manne ya Pemba ulikua umeshakamilika kabla ya zoezi hilo kusitishwa, na kuishauri Tume ya Uchaguzi kukamilisha zoezi hilo na kumtangaza mshindi.
 

Aidha ameelezea kusikitishwa na kitendo cha kuchukuliwa kwa nguvu kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Abdulhakim Muhsin Ameir, sambamba na kutoonekana kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo katika kituo cha majumuisho ya matokeo hayo kilichoko Bwawani hadi alipotoa kauli hiyo, pamoja na kutoonekana kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi nd. Salim Kassim Ali.

Baadae Mgombea huyo wa Urais kupitia CUF alizungumza na wafuasi wa Chama hicho nje ya Ofisi hizo za makao makuu Mtendeni, na kuwataka kuwa watulivu na kuendeleza amani wakati Chama kikiendelea kufuatilia haki zao. 

Aliwataka wafuasi hao kutokuwa na wasi wasi wa ushindi, na kwamba haki yao hiyo itapatikana ndani ya kipindi kifupi kijacho.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588

2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na waajiriwa wapya katika Ufunguzi wa Semina Elekezi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara Rasilimali watu Bw. Said Msambachi ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi. Aurelia Matagi , ( wa kwanza kushoto) , Kwa upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro Kimwaga pamoja Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro.
3
Baadhi ya Watumishi wapya walioajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika Ufunguzi wa Semina Elekezi ya Waajiriwa wapya iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
4
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi Aurelia Matagi ( kulia) akiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi Bw. Safari, wakiwa wanatoa maelekezo ya kujaza fomu za kuajiriwa katika Semina Elekezi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro ( kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu Bw. Said Msambachi ( kulia) mara baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Meru kuwasili katika ufunguzi wa Semina Elekezi ya waajiriwa wapya iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.



                                                                                               Na Mwandishi wetu

Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ajira mpya kwa Watumishi wapya wapatao 588 ikiwa idadi kubwa miongoni mwao ni Watumishi wa kada ya Afisa Wanyamapori na Wahifadhi wanyamapori lengo likiwa ni kukabiliana na mashambulio mengi kutoka kwa majangili.
 

Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa waajiliwa wapya hao yaliyofanyika leo katika Chuo cha Taifa cha Utalii katika Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Dkt. 

Adelhelm Meru amesema watumishi hao ni lazima wajitume ili kukidhi malengo kwa kudhibiti na kusimamamia matumizi endelevu ya wanyamapori pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira ya mapori ya akiba.
 

‘’Fursa hii mliyoipata isaidie kuongeza chachu na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa kuhakikisha kuwa Maliasili tulizonazo zinalindwa na kutunzwa kikamilifu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye’’ Dkt. Meru alisisitiza.
 

Amewataka watumishi hao kufanya doria katika maeneo ya mapori ili kuimarisha uwepo wa Wanyamapori katika maeneo ambayo Watalii wanaweza kupata fursa ya kuwaona kwa urahisi zaidi.
 

Aliongeza kuwa Watumishi hao ni lazima waweke nguvu na mikakati endelevu katika kupambana na uchomaji moto ovyo wa mapori, kilimo na uingizaji wa mifugo katika maeneo ya mapori yaliyotengwa kwa ajili ya Wanyamapori
 

Pia aliwataka Watumishi hao kujiepusha na na tabia ya kupokea rushwa hasa kwa watumishi walio kwenye Mapori ya akiba, mapori tengefu na vituo vingine vya kazi na Mtumishi yeyote atakayethibitika kupokea rushwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza ajira yake.
 

Aidha, Dkt. Meru amewaasa watumishi wapya kujiepusha na anasa na ulevi wa kupindukia likiwemo janga la Ukimwi ambalo limekuwa sio rafiki kwa nguvu kazi ya taifa ambayo imepatikana kwa gharama kubwa
 

Watumishi wapya wapatao 588 walioajiriwa ni Maafisa wanyamapori daraja la pili 111, Maafisa Utalii daraja la pili 17, Wahifadhi wanyamapori daraja la pili 14, Wahifadhi Wanyamapori la pili tatu 433.

Wengine ni Wahasibu wasaidizi 11, Msaidizi wa Maktaba 1 na fundi sanifu Umeme 1, Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu.
 

katika idara mbalimbali wakiwemo, wahifadhi wa wanyamapori daraja la (2) 14, wahifadhi wanyamapori daraja la (3) 433 uhasibu wasaidizi 11, fundi umeme 1, maofisa utalii daraja la (2) 17, msaidizi wa Maktaba 1, leo Asubuhi katika ghafla ya kuwa karibisha na kuwapa mafunzo waajiliwa hao iliyofanyika jijini Dar es salaam katika chuo cha utalii kilichopo Temeke. Dkt. 

Meru alisema, rushwa ni tatizo kubwa katika Taifa letu hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii haina budi kuwa mfano wa kuigwa katika kupiga vita rushwa na kutatua matatizo ya wafanyakazi hasa kwa watumishi walio kwenye Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na vituo vingine vya kazi.

Pia aliongezea nakusema, napenda nimalizie kwa kuzumzia kwa kifupi tatizo lingine linalokabili Taifa letu, Tatizo hili ni janga la ukimwi. Uboreshaji wa utendaji kazi katika utumishi wa Umma hususani ulinzi wa Wanyamapori hauwezi kufanikiwa ikiwa janga la Ukimwi halitadhibitiwa. 


UKIMWI unasababisha vifo vya watumishi hivyo kulipunguzia Taifa nguvu kazi ambayo imepatikana kwa gharama kubwa, kwa hiyo kila mmoja wenu anatakiwa ashiriki kikamilifu katika kujikinga na janga hilo na kuchukua tahadhari kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. 

Wizara itaendelea na jukumu lake la kuelimisha wafanyakazi kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI.
 

Pia mmoja wa waajiliwa hao nae alimshukuru katikbu Mkuu kwaniaba ya waajiliwa wenzake na kuahidi kuwa watafanya kazi kikamilifu, watakuwa waadilifu na watashirikiana na wafanyakazi wengine wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

KURASA ZA MAGAZETI YA HARDNEWS NA BURUDANI ALHAMISI OKTOBA 29,2015

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.