Mamlaka za nchini China zinachunguza
tukio jipya la mlipuko katika mkoa wa Guangxi, ikiwa ni siku moja tu
kupita tangu mfululizo wa milipuko 17 kuua watu saba.
Shirika la habari la umma limesema
mlipuko huo umetokea katika nyumba majira ya saa mbili saa za nchini
China, katika kaunti ya Liucheng.
Matukio 17 ya milipuko imelikumba
eneo la Liucheng siku ya jana, ambayo polisi wanaamini ni mabomu
yaliyowekwa kwenye barua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni