Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza
Manchester United wamepata ushindi wao wa kwanza katika Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya katika hatua ya makundi baada ya kutoka nyuma na kuibuka
na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya VfL Wolfsburg.
Wakati Chelsea pamoja na Arsenal
zikiwa zimepoteza michezo yao jumanne, United walikuwa katika hatari ya
kufuata nyayo zao baada ya Daniel Caligiuri kufunga bao lililozaliwa
kutokana na pasi sita.
Hata hivyo Juan Mata aliisawazishia
Manchester United kwa mkwaju wa penati uliotokana baada ya kumnawisha
mpira beki wa Wolfsburg, na kisha Chris Smalling akiunganisha pande
la nyuma la Mata na kuandika bao la pili.
Wayne Rooney na Anthony Martial wakianzisha mpira baada ya kufungwa bao la kwanza
Chris Smalling akipachika wavuni bao la pili la Manchester United
Nyota Cristiano Ronaldo ameifikia
rekodi ya Raul ya kuifungia Real Madrid kwa kuifungia magoli mengi na
kufikisha idadi ya kupachika magoli 500 kwa kufunga mabao mawili
dhodi ya Malmo nchini Swedeni.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka
Ureno aliandika bao la kwanza katika mchezo huo wa Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya wa kundi A, kwa kuunganisha pande alilopewa na Isco na
kisha baadae kupachika tena bao la pili.
Matokeo mengine ni Borussia
Mönchengladbach 1 - 2 Man City, Shakt Donsk 0 - 3 Paris St G, CSKA 3
- 2 PSV, FC Astana 2 - 2 Galatasaray pamoja na Atl Madrid 1 - 2
Benfica.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni