Serikali ya mpito ya Burkina Faso
imesema jeshi limetwaa kampi za walinzi wa rais waliofanya mapinduzi
mapema mwezi huu.
Maafisa wa jeshi wametangaza
kutwaliwa kwa kambi hizo katika taarifa yake iliyotolewa kwenye
runinga, hata hivyo haikuelezwa iwapo kunawatu waliouwawa ama
kujeruhiwa.
Awali waandishi wa habari waliopo
katika Jiji la Ouagadougou wamesema milio ya risasi na milipuko
imesikika huku moshi ukitapakaa juu kwenye kambi za walinzi hao wa
rais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni