Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
atasimamia mwenyewe wizara inayosimamia sekta muhimu ya mafuta,
wakati huu akiwa amebakiwa na siku chache tu za kutangaza baraza lake
la mawaziri.
Taarifa kutoka Jijini New York
Marekani ambapo Buhari anahudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
zimemnukuu rais huyo akisema yeye atakuwa rais wa wizara ya
rasilimali ya mafuta, jambo ambalo limethibitishwa na msemaji wake
Femi Adesina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni