Kocha Jose Mourinho amekiri kuwa
hatambui ni kikosi gani chake ni kizuri kwa sasa baada ya kupata
kipigo cha tano katika msimu huu, wakati kocha huyo aliporejea jana
kupambana na timu yake ya zamani ya FC Porto.
Hata hivyo Mourinho ametetea uamuzi
wake wa kuwaacha nyumbani washambuliaji wake Radamel Falcao pamoja na Loic Remy
na kuifanya timu yake kuwapo ugenini na washambuliaji wasiotambulika
katika benchi, ingawa amesema uamuzi huo sio wa adhabu.
Pia kocha huyo ametetea uamuzi wake
wa kuwaweka benchi Eden Hazard na Nemanja Matic pamoja na kumuacha
Oscar Jijini London, ingawa amekiri kiwango cha Chelsea cha sasa si
cha kuitegemea kudumu katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni