Mapigano makubwa yanaendelea katika
mji wa Kunduz nchini Afghanistan siku moja baada ya vikosi vya
serikali kuanzisha mashambulizi kuutwaa mji huo kutoka kwa Talibani.
Mashambulizi mawili ya angani
yaliyofanywa na Marekani siku ya jana yamesaidia kusitisha nguvu ya
wapiganaji watalibani kutwaa uwanja wa ndege ambao ndio ngome kuu ya
jeshi la Afghanistan.
Shirika la ujasusi la Afghanistan
limesema mashambulizi hayo yamemuua kiongozi wa mkoa wa kundi la
Taliban na makamu wake, hata hivyo Talibani wamekanusha taarifa hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni