Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
|
Na Jamiimojablog.
Watu watano wamefariki dunia
Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la ajali ya haice
iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza gari lenye
namba za usajili T.519 Akh aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na
dereva asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili
T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.
Ajali hiyo imetokea Septemba 29
majira ya Saa 4 usiku katika eneo la Nane-Nane, Kata Ya Isyesye,
barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu
Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha
pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine
watatu raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara
moja ambao walikuwa wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo kwa
mtindo maarufu wa Mshikaki.
Aidha Katika ajali hiyo Edward
Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye Haice
alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.
Amesema dereva wa hiace alikimbia
mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka
zikiendelea kufanyika na jeshi hilo miili ya marehemu imehifadhiwa
Hospitali Ya Rufaa Mbeya.
Katika tukio jingine mtu mmoja
Mkazi wa Masoko Wilaya ya Rungwe Ndugu Tukupyelesya Enock
Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa
wakisafiria T.913 Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva
asiyefahamika kuacha njia na kupinduka huko katika kijiji cha
Masoko, Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya
Tukuyu/Lwangwa.
Aidha Katika ajali hiyo abiria
Watatu wanawake wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw
katika hospital ya Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha .
ajali hiyo ni mwendo kasi dereva .
Kufuatia matukio hayo Kamanda wa
Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed
Msangi ametoa o wiito Kwa madereva kuwa Makini wanapotumia vyombo
vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni