MAGUFULI AITEKA ARUSHA,APOKELEWA KWA KISHINDO

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za CCM,Ndugu Ole Sendeka akiwahutubia maelfu a wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.
Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Umati wa Wakazi wa jiji la Arusha na Vitongoji vyake wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli jijini humo.
Wananchi wa Arusha waliofurika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakionesha kufurahia Sera za Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Arusha mjini,Ndugu Phillemon Mollel mbele ya maelfu ya  wakazi wa jiji la Arusha kwenye mkutano wa kampeni
Wakazi wa maeneo ya Jirani na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid waliacha Shughuli zao na Kufuatilia sera za Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.
Baadhi ya Wanachama wa Chadema wakirejesha kadi zao kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya wakitumbuiza katika Mkutano huo wa kampeni.
Hapa ni kazi na dawa.......
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Monduli,Namelok Edward Moringe Sokoine kwenye mkutano wa kampeni ulofanyka mjini Monduli mapema leo mchana.
Mgombea Ubunge jimbo la Monduli,Namelok  Edward  Moringe Sokoine akitabasamu mara baada kunadiwa na Mgombea Urais wa CCM Dkt Maguli mbele ya wakazi wa mji wa Monduli (hawapo pichani) mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli (wa pili kushoto),akiwa ameambatana na baadhi  ya wajumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni ya CCM,wakishiriki sala ya pamoja ya kumuombea Marehemu,Waziri Mkuu wa zamani,Hayati Edward Sokoine Moringe kwenye kabuli lake,Monduli juu,mkoani Arusha.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiweka shada la Maua kwenye kabuli la Waziri Mkuu wa zamani,Hayati Edward Sokoine Moringe,ambapo pia akiwa na baadhi  ya wajumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni ya CCM,walishiriki sala ya pamoja ya kumuombea Marehemu,
 Mke wa Marehemu Sokoine akisaidiwa kuweka shada la maua
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mtoto wa Marehemu,Hayati Edward Moringe Sokoine wakitoka nje ya Kabuli la Hayati Sokoine mara baada ya kushiriki sala ya pamoja,Monduli juu mkoani Arusha.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni mjini Longido,mkoani Arusha
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wakazi wa mji wa Longido,mara baada ya kuwahutubia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni