-Wasanii wa Tanzania Ali Kiba,Fid Q na Vanessa kuwasha moto
Wasanii
nguli kutoka Tanzania wataungana na wasanii wengine 27 barani Afrika
katika msimu wa tatu wa maonyesho ya burudani ya muziki maarufu kwa
jina la Coke Studio Afrika ambalo litaanza Jumamosi wiki hii .Onyesho
la mwaka huu ni tofauti na yaliyopita kwa kuwa litaendana na mabadiliko
yaliyopo katika muziki duniani “Kolabo”na litarushwa na kituo cha
televisheni cha Clouds kuanzia saa 12 jioni.
Meneja
wa Biashara za Coca-Cola nchini Maurice Njowoka amesema kolabo ya
wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba
nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika
hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga
muziki mchanganyiko lakini safari hii utatumika katika onyesho la Coke
Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali
barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za
uimbaji”.Alisema
Wasanii
wanne kutoka Tanzania watakaokuwa kwenye Kolabo la Coke Studio mwaka
ambalo onyesho lake litaanza kuonekana kwenye luninga Jumamosi ya Oktoba
10 ni Ben Pol ambaye atakuwa pamoja na mwanamuziki nguli kutoka Kenya
anayejulikana kama Wangechi,Fid Q atakuwa pamoja na Maurice Kirya
kutokana Uganda,Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba atashirikiana na
Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na Vanessa Mdee atakuwa pamoja na
mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.
Maandalizi
ya kuanza kwa msimu mpya wa Coke Studio Afrika yamekamilika na wapenzi
wa muziki nchini wanasubiri kwa hamu kuwaona wanamuziki wanaowashabikia
wakiwasha moto kwa kushirikiana na wanamuziki kutoka nje ya nchi na hii
inadhihirisha kuwa onyesho la Coke Studio litaacha historia ya pekee
katika fani ya muziki nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni