Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet,
John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya
Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa
kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo
kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja,
Christina Kausan.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri
wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia
ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi.
Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo
na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na
waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya
usafiri hapa nchini.
Alisema kuwa ndege hiyo ina uwezo wa
kubeba abiria 108 aliongeza kuwa zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa
nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.
Aliongeza kuwa kwa kuwa Fast jet hapa
nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo kwa kuwa hazitumii
matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.
" Hii imetokea tu kuwa wakati serikali
imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta mengi na sisi tulikuwa pia
tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi naona kuwa watanzania
watanufaika zaidi" alisema Corse.
Pia aliipongeza serikali kwa kuleta
ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa,
Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet hazifiki.
Alisema kwa kuwa lengo la Fast jet ni
kuwapatia watanzania huduma nafuu za usafiri wa anga hivyo inafurahia
pale ambapo inaona kuwa ndege za serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet
haifiki.
Alisema kuwa kwa kupeleka ndege kwenye
mikoa hiyo ni hatua ambayo inatimiza lengo la Fast jet la kuhakikisha
watanzania wanapata huduma bora za anga kwa bei rahisi na kwa wakati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni