BINTI WA ASKOFU TUTU AVULIWA UCHUNGAJI KWA NDOA YA JINSIA MOJA

Binti wa Akofu Mstaafu Desmond Tutu, amelazimika kuachia madaraka ya uchungaji wa Kanisa la Anglikana la Afrika Kusini baada ya kumuoa mwanamke mwenzake.

Mchungaji Canon Mpho Tutu-van Furth hawezi kupokea mkate wa bwana na hatoruhusiwa kufungasha ndoa, kubatiza ama kuzika, na amerejesha kanisani leseni ya uchungaji.

Mchungaji huyo Canon Mpho Tutu-van Furth amesema baba yake Askofu Mstaafu Tutu na amechukizwa na kitendo chake lakini hakushangazwa na ndoa hiyo.
                 Canon Mpho Tutu-van Furth akiwa na baba yake Askofu Mstaafu Tutu

BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPITISHWA, USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA TANZANIA WAPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 3

 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Baadhi ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo
imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akimweleza jambo Mbunge wa Bunda mjini Mhe. Esther Matiku (CHADEMA) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni mjini Dodoma.

 

                                                                              Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

                                                                                                  Dodoma.

Serikali imesimamisha utoaji wa vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.

Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia mazingira ya uhifadhi wa wanyama hao.

                                           USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA NCHI.

Amesema kumekuwa na taarifa za baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama hao.

Kuhusu wanyama wanaoruhusiwa kusafirishwa kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema kuwa wamekuwa wakisafirishwa kinyume na utaratibu na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.

Amesema makampuni hayo yamekuwa yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.


                          UTALII KUSINI MWA TANZANIA NA MAENEO MENGINE.

Amesema Serikali itatekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa Utalii wa Kusini ili kuweka mazingira wezeshi na kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikisababisha watalii kushindwa kufika katika maeneo ya hifadhi za Taifa eneo la ukanda wa kusini mwa Tanzania.

Baadhi ya maeneo yatakayoshughulikiwa ni gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi katika maeneo hayo kuwa kubwa hadi kufikia Dola za kimarekani 1800 jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa watalii hao.

Amesema Serikali itaanzisha vituo vya kuwekea mafuta ya ndege mahali vilipo vivutio vya utalii ili kuziwezesha ndege ndogo kufika kwa urahisi na kupata huduma ya kuongeza mafuta ili kupunguza gharama kwa wasafiri wanaotembelea hifadhi za eneo hilo.

Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itanunua ndege ndogo abiria ili kuwezeha watalii kufika kwa urahisi katika maeneo ya hifadhiza Taifa.

                                                      UTAMBUZI WA MAENEO MAPYA YA UTALII.

Serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya, mikoa na Wabunge itaanzisha mpango mpya kuviorodhesha vivutio vyote vya utalii vilivyo katika maeneo yao ili viweze kutangazwa ipasavyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mpango huo itaandaliwa orodha ya vivutio hivyo ili vianzwe kutangazwa rasmi.

Katika kuimarisha shughuli za utalii nchini serikali itaweka mkazo katika uimarishaji wa utalii wa utamaduni, uimarishaji wa maeneo ya historia na Malikale ili kuwezesha eneo hilo kuchangia zaidi katika pato la taifa.

                                                  ULINZI NA USALAMA WA HIFADHI ZA TAIFA.

Prof. Maghembe ameeleza kuwa suala la ulinzi na usalama wa hifadhi zote za Taifa liko kwa mujibu wa sheria na kubainisha kuwa serikali imeanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) litakalochukua mbuga zote zilizokuwa na uongozi ambazo ziko nje ya TANAPA.

Jeshi hilo litapambana kikamilifu na ujangili, kuimarisha maadili na nidhamu ya askari wa ulinzi wa hifadhi za taifa pamoja na kushughulikia maslahi yao na kuondoa migogoro kati ya askari na wananchi.

Amesisitiza kuwa mara baada ya Bunge la Bajeti, Wizara itakutana na wahifadhi wakuu wote ili kuweka vigezo vya kuzingatia katika majukumu yao na kusisitiza kuwa wahifadhi wote watakaoshindwa kwenda na kasi ya vigezo vilivyowekwa hawatajumuishwa kwenye jeshi hilo.

Aidha, amekemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi kupiga raia na kuchoma nyumba za wananchi kuwa havikubaliki na ni kinyume cha majukumu yao.

” Nimesikiliza kwa makini michango ya wabunge na nimesikia wafanyakazi katika hifadhi zetu wanapiga raia wanaua mifugo na kuchoma nyumba za wananchi jambo ambalo halikubaliki, hatukuwatuma kufanya hivyo” Amesisitiza Prof.Maghembe.

                                                  MIGOGORO YA MIPAKA MAENEO YA HIFADHI.

Serikali imesema mpaka sasa kuna migogoro ya ardhi 281, kati ya hiyo 35 ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ni migogoro ya hifadhi na kuita Mikoa yenye migogoro hiyo kuwa ni pamoja na Mara , Tanga na Kagera inachukua jumla ya asilimia 50.

Aidha, amesema kuwa mkoa wa Tabora unaongoza kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi na unaongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya hifadhi kwa asilimia 40.

Katika kuishughulikia migogoro hiyo Serikali imeziagiza wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana pamoja katika kutatua migogoro yote ya ardhi nchini.

UBORESHAJI WA MAENEO YA HIFADHI NA MAMLAKA ZA UHIFADHI.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kushughulikia usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya kisasa katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro vitakavyokuwa na uwezo wa kugeuza maji taka kuwa poda ili kuweka mazingira yote ya mlima huo kuwa safi.

Aidha,amesema kuwa Mamlaka za hifadhi za Taifa zimeendelea kuchangia katika maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, miundombinu ya barabara, utoaji wa madawati katika halmashauri mbalimbali nchini.

RAIS DKT. MAGUFULI AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUWA WAZALENDO

mg3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya Kazi.
mg1
Baadhi ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg5
Kaimu Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.
mg6Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi wenye nia ya kuwakwamisha.
mg7
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi mbalimbali za ujenzi nchini.
mg8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg10 mg11
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Wakandarasi na viongozi wa mkoa wa Wizara ya Ujenzi wa mkoa wa Dar es salaam.
mg12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Picha na ikulu

DKT. SHEIN AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MPYA WA MUUNGANO WA VISIWA VYA COMORO LEO

Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kulia) alipokuwa akiapishwa na Jaji wa Mahkama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (wa tatu kushoto) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro leo kufuatia ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio Mei,11 mwaka huu
Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri alipokuwa akiapishwa na Jaji wa Mahkama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (hayupo pichani ) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro leo kufuatia ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio Mei,11 mwaka huu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani Boinakheri, baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio Mei,11 mwaka huu, katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro leo
Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kulia) alipokuwa akiapishwa na Jaji wa Mahkama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (wa pili kushoto) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro leo kufuatia ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio Mei,11 mwaka huu
Rais mstaafu wa Muungano wa Comoro Dkt.Ikulilou Dhoinine akimkabidhi Bendera ya Nchi kama ishara ya kumakabidhi madaraka Rais Mpya wa Nchi hiyo Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kushoto) baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio Mei,11 mwaka huu,sherehe ya kuapishwa Rais huyo ilifanyika leo katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro
Wageni mbali mbali na Viongozi wa nchi ya Comoro wakiwa katika sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kushoto) baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mey 11 mwaka huu,sherehe ya kuapishwa Rais huyo ilifanyika leo katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,[picha na Ikulu.]26 Mei 2016.

EAC TABLES USD 100 M BUDGET TO EALA

 Hon Dr Susan Kolimba, Deputy Minister, Foreign Affairs and East African Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko
The deputy Minister of Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.

The EAC today presented Budget estimates for the Financial Year 2016/2017 totaling $101,374,589 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha. Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon Dr Susan Kolimba presented the Budget speech to an attentive House on behalf of the substantive Minister and Chair of the EAC Council of Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.

The 2016/2017 Budget is a drop down from $110,660,098 Million presented to the House in the previous Financial Year. The Budget prioritizes the full implementation of the EAC Single Customs Territory, enhanced implementation of the EAC Common Market Protocol especially additional commitments and interconnectivity of border immigration systems and procedures across Partner States and enhancement of productivity and value addition in key productive sectors.

The budget also takes cognisance of development of cross-border infrastructure and harmonisation of laws, policies and standards in respective sub-sectors, implementation of a liberalised EAC airspace, enhanced implementation a One Area Network in telecommunications and the implementation of EAC Peace and Security initiatives.

According to the Minister, other key specific priorities are strengthening of the legal and judicial systems, enhancement of Information, Communication and Education to promote popular participation of the citizenry in the EAC integration process and promotion of education, science and technology for creative and productive human resources.

The Chair of Council termed the establishment of a policy framework and institutional structures for establishment of the EAC Political Federation as another key priority area in the coming financial year.

The Budget is allocated to the Organs and Institutions of the EAC as follows; East African Community Secretariat ($57, 872, 785), East African Legislative Assembly ($16,034,324) and the East African Court of Justice ($4,286,477).

The Inter-University Council for East Africa shall receive ($4,553,890), Lake Victoria Basin Commission ($11,214,708) while $ 2,131,422 is earmarked for the Lake Victoria Fisheries Organization. On their part, the East African Science and Technology Commission shall receive ($ 1,161,438), East African Kiswahili Commission ($ 1,134,542) and the East African Health Research Commission ($ 1,397,438). The East African Competition Authority is to benefit from $587,565 in the Financial Year.

The 2016/2017 Budget is to be financed by Partner State contributions ($47,565,377) compared to USD 47 566,973 in the current Financial Year; Development Partners support ($46,717,601) which is a significant drop from USD 58,555,635 of the previous year. The Member Universities will inject USD 431, 923, General Reserves USD 6, 354, 248 and miscellaneous revenue USD 305, 440.
The EAC Political Federation is yet a key priority area on the agenda in the coming Financial Year as the mode of the regional Constitution making process commences. The same applies to strengthening of regional and international relations through mobilisation of Partner States’ diplomatic missions and the East African diaspora for effective participation in EAC integration processes and building of multilateral/international networks in pursuit of EAC objectives.

The Minister highlighted a number of achievements registered in the Financial Year 2015/2016, notably, the upscaling of the Single Customs Territory (SCT) through finalisation of operational instruments of the business manuals, deployment of SCT Monitoring and Evaluation tools and deployment of staff in some Partner States. The Minister remarked that 10 out of the 15 One Stop Border Posts were already operational.

The chair of the Council of Ministers further stated that the EAC Elimination of Non-Tariff Barriers Bill (NTB), 2015 passed by EALA was undergoing assent and would spur business and enhance the free movement aspects. The Minister told the House that National Monitoring Committees on NTBs and the EAC Regional Forum on NTBs had continued to spearhead the elimination of NTBs affecting Intra-EAC trade.


According to the Minister, the Council of Ministers further appointed Commissioners to the EAC Competition Authority. “The Authority is set to commence operations in the financial year 2016/17 and it will act as a one stop centre in the enforcement of provisions of the EAC Competition Act. The Secretariat has finalized preparations for the operationalization of the East African Competition Authority”, the Minister said.

In order to strengthen the Monetary Union, the Minister said draft Bills for the establishment of the East African Monetary Institute and the East African Statistics Bureau were been developed and negotiated by the Partner States. The Minister informed the House that in a bid to harmonise tax regimes, the EAC Secretariat had continued with efforts for closed co-ordination of fiscal policies with focus on critical areas for harmonisation.

“So far, domestic Tax Harmonization Policy has been drafted by the Secretariat and is being peer reviewed by the International Monetary Fund (IMF) before submission to the relevant Organs of the Community for consideration” the Minister said.

Under Infrastructure development, the Minister informed the House of on-going construction works especially on the Northern Corridor. The Minister said the Arusha-Holili/Taveta-Voi road project and the second multinational road projects in the region had commenced.

“In addition, the Secretariat signed a grant agreement amounting to US$ 2.68 million in November 2014 with the AfDB through the NEPAD Infrastructure Project Preparation Facility (NEPAD-IPPF) for the feasibility studies and detailed designs of two key links for the Republics of Rwanda and Burundi to the Central Corridor. These are the 250km long Nyakanazi – Kasulu – Manyovu road in Tanzania linking to the 78km long Rumonge –Bujumbura road in Burundi, and the 92km long Lusahunga – Rusumo road in Tanzania linking to the 70km long Kayonza – Kigali road in Rwanda”, the Minister said.

Hon Dr Kolimba further remarked that progress with regards to the construction of the Mombasa-Nairobi Standard Gauge railway stood at approximately 70% as at March 2016.

On Industrialisation and SMEs Development, the Chair of Council said that the EAC had developed a draft Industrialisation Bill and that it was awaiting legal scrubbing and input before it is presented to the Sectoral Council on Legal and Judicial Affairs for consideration.

Within the Energy Sector, the Minister informed an attentive House that implementation of power projects under the East African Power Master Plan had resulted in the addition of 425 MW over the last two years raising the region’s installed capacity from 4,468 MW to 4,893 MW against a peak demand for 3,326 MW for the inter-connected system last year.

In the Tourism and wildlife sector, the Minister informed the House that a regional strategy to combat poaching and illegal trade in wildlife and wildlife projects was been developed by the Secretariat.

“In the next financial year, 2016/17 the priorities for the Tourism and Wildlife sector will include, among others, developing guidelines for smooth cross border tour operations, implementation of the regional strategy to combat poaching and the illegal trade in wildlife and wildlife products, finalizing the development of a tourism legal framework, training of more hotel assessors from Partner States and transferring training program of hotel assessors to training colleges in hospitality in Partner States”, the Minister remarked.

On health matters, the Minister informed the House of progress in promotion of integration of health sector and interventions to address challenges facing the sector in line with Article 118 of the Treaty.

“Mr. Speaker, in order to strengthen human resource for health and ensure right skills and knowledge is provided by the various public and private sector universities and other institutions of higher learning in the fields of medicine, medical laboratory sciences, nursing, pharmacy, dentistry and other health professions, regular joint inspections have been conducted by EAC Secretariat in collaboration with the EAC Partner States’ National Health Professional Boards and Council using regional guidelines and checklists developed for the inspection and mutual reciprocal recognition”, the Minister said.

On the Common Market, the Chair of Council remarked that the region was keen to ensure implementation of the Protocol. “Mr. Speaker, this August House may be pleased to note that during the 17th Ordinary Sitting of the Summit of EAC Heads of State, the new International East African Electronic Passport was launched. The East African e-Passport represents; the ordinary; official/service anddiplomatic Passports. The introduction of the new e-Passport is a milestone that will see our Partner States join global initiatives where over 100 countries are implementing the electronic passports”, the Minister said.

“The Partner States are expected to issue the new international EA e- passport in to their citizens in January 2017 and make necessary arrangements with relevant authorities to implement the passport”, he added.

The Minister remarked that consultations with stakeholders in the employment subsector such as the East African Trade Union Confederation (EATUC) and Employers’ Associations have been undertaken on the process of harmonization of the work/residence permit fees pursuant to Regulation 6(9) of the East African Common Market (Free Movement of Workers) Regulations Annex II and regulation 6(5) of the East African Community Common Market (Right of Residence) Regulations.

On matters of political affairs, the Minister informed the House of steps been taken to lay ground for political integration. The 31st Meeting of the EAC Council of Ministers in May 2015, the Minister said, established a Sub-Committee of Ministers Responsible for EAC Affairs to consider the concept note, Terms of Reference (ToRs); Roadmap for the Constitution Making Process, and; to determine the Model of the EAC Political Federation for consideration. The Sub-Committee met in February 2016 and made a report to the Council on the basis of which the Council reported to the 17th Ordinary Meeting of the Summit. The report was to the effect that the Partner States had generated convergence on a Confederation as the Model of the East African Federation.

The Minister said that the Community was keen to ensure regional peace and security initiatives are realized. The sector players have a critical role in ensuring the facilitation of the enjoyment of freedoms and rights guaranteed by the Treaty. The sub-sector continued regular consultations towards joint action against Terrorism, Small arms and Light weapons trafficking, human and narcotics trafficking, theft of motor vehicles and other cross border crimes. To this extent a training manual and operating procedures on public order management with a human rights perspective at the 14th Eastern Africa Police Chiefs Cooperation Organization – Annual General Meeting (EAPPCCO- AGM) was launched, the Minister informed the House.

“The next financial year will be dedicated to conclusion of another three harmonized Standing Operating Procedures remains an omnipresent threat to the enjoyment of these freedoms and rights. Attention will be paid to transnational crimes that feed terrorism and terror infrastructure”, he said.

In a bid to improve financial management and reporting, the Minister remarked that the Secretariat has rolled over the Sun systems to all EAC institutions which were prior to, using different financial management systems. The Budget Management System (BMS) which was developed and installed was as well rolled out to all EAC Institutions, making it easy to prepare Annual Operational Plans, MTEF budget and monitor its execution. As a result of these improvements, budgets and financial reports are timely, well prepared and submitted, the Minister said.

MATUKIO MBALIMBALI YA PSPF-INTER COLLEGE BONANZA


 Picha mbalimbali zikionyesha matukio mbalimbali yaliyojiri katika tukio  la PSPF INTER -COLLEGE BONANZA lililofanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu jijini Arusha mwishoni mwa wikii liyopita ambalo lilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wanachuo mbalimbali kuhusu mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF(picha na mahmoud ahmad,Arusha





JUMLA YA WATUMISHI HEWA 132 WILAYANI ARUMERU WASHIKILIWA



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Felix Ntibenda (picha ya maktaba)

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Wilson Nkhambaku, ametangaza kubaini na kuwashikilia watumishi hewa 132 ambao wamepatikana kutoka Halmashauri za Arusha na Meru zilizopo kwenye Wilaya hiyo.

Aidha, Nkhambaku amesema bado wanaendelea kuwahoji huku uchunguzi zaidi ukiendelea, na kwambw tayari akaunti zao zimefungwa lengo likiwa ni  kudhibiti kutoingiziwa tena  fedha.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la  Madiwani Halmashauri ya Arusha, Nkhambaku alisema kati ya hao, 28 wanatoka katika Halmashauri ya Arusha na waliobaki wanatoka Halmashauri ya Meru.

Alisema kufuatia hatua hiyo, tayari Wilaya imesharudisha zaidi ya Sh milioni 70, baada ya watuhumiwa wote  kujisalimisha na kurejesha fedha hizo, na kwamba zaidi ya milioni 10 zimepatikana Halmashauri ya Arusha na nyingine Halmashauri ya Meru.

Nkhambuka aliongeza kuwa mara  baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa wote  watakaobainika watafikidhwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi wa nchi.

EALA SWEARS IN SECRETARY GENERAL LIBERAT MFUMUKEKO


 The Clerk to the Assembly administers the oath to the EAC Secretary General, Amb Liberat Mfumukeko 
 The EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko signs the oath of Allegiance to the House
 CONGRATULATIONS: The EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Kidega offers his congratulations to the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko moments after taking the Oath
 The EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko is led in to the House to take the Oath of Allegiance by the Clerk to the Assembly, Kenneth Madete. At back is Hon Hafsa Mossi and Hon Isabelle Ndahayo (photo by Mahmoud Ahmad,Arusha )
 Hon. Abdallah Mwinyi addresses the Assembly
Hon Shyrose Bhanji contributes to the debate in the House

SEREKALI YAPOTEZA KODI NYINGI


mbunge wa bunge la Afrika mashariki Shyrose Bhanji akiongea katika bunge hilo jijini Arusha jana kuelezea wigo mapana unatakiwa ili serikali isipoteze kodi

Na Mahmoud Ahmad,Arusha


 Serekali imekuwa inapoteza kodi nyingi  zinazotokana  na ushuru wa mazoao kutokana na kuwa na mzabuni  mmoja ambaye anakusanya  kodi za mazao  kwa nchi nzima .

Hayo yamebainishwa na  mbunge wa  EALA, Shy-Rose  Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge hilo   ambapo alisema kuwa kuna changamoto kubwa  ya utekelezaji wa umoja wa forodha hapa nchini Tanzania.

Alisema kuwa  wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali  zinazofikia kiwango   staili cha asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa awatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao katika  nchi za jumuiya wanachama .

 Aidha alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande  wa Tanzania kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi  au kubaini viwango vya kusamehewa kodi zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya tccia.

Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa  upya katika nchi yetu na serekali kwasababu TCCIA aipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni mikoa tu  huku katika ngazi za wilaya pamoja na vijiji awapatikani.


Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na pia wananchi wengi  pamoja na wafanya biashara wengi kutokujua dhamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha mfanyabiashara kujua unafuu wa wa kodi.


“sasa ivi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa  dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa jukumu la kutoa hati  hizi kwa wadau wengine ili kuleta unafuu wakodi “alisema Bhanji


Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za biashara za manispaa pamoja na  ofisi za biashara za  wialaya nawao waweze kupewa  ili jukumu na wao waweze kutoa hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM MKUTANO WA ADB – LUSAKA


lu1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
lu3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu4Rais wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lu8Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIJANA WATAKIWA KUACHANA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA


Muandaaji wa tamasha la michezo kwa vijana wa mkoa wa Arusha Neema Mollel ambaye pia ni  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina pamoja na  mlezi wa Timu za mpira kata ya Sakina Jijini Arusha akiongea katika fainali za Tamasha la vijana lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
 
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Olmatejoo A.
 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Diwani wa kata ya Ungalimited akiwa anawaasa vijana kuachana na madawa ya kulevya katika fainali hizo
 
Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.
 …………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
 
Timu ya Intersport Club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana  mara baada ya  kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.
 Tamsha hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi kikubwa 
Akizungumza wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na kuwapa elimu  ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana 
Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo
 
 “nia alisi ya  kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira”Alisema Neema Mollel
 
Aidha aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na
jamii.
 
Akikabidhi kombe kwa washindi ambao ni Interspot Club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.
 
Sambamba ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na  Tsh 100,000 ,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black Eagle Tsh 50,000.