Na Francis Godwin
ASKOFU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegela amewapongeza
waumini wa Dayosisi hiyo kwa kumpata askofu mpya atakayechukua
nafasi yake pasipo kuwepo kwa vurugu za aina yoyote tofauti na
maeneo mengine ambayo pindi linapotokea zoezi la uchaguzi wa askofu
huwa na vurugu kubwa .
Huku
akisema kuwa hana ugomvi wowote na askofu wa Dayosisi Kusini
Isaya Mengele kama ambavyo watu wanasema na kuwa mgogolo
unaoendelea kati ya askofu huyo na waumini wake wa jimbo la
Mufindi utatuzi wake ni maombi na sio kutumia nguvu. Alisema
tayari amepokea maombi ya waumini wa jimbo la Mufindi kutaka
kuhamia dayosisi ya Iringa na hana sababu ya kuwakataa kuwa pindi
watakapokuwa tayari atawakaribisha.
Askofu
Dr Mdegela aliyasema hayo leo wakati wa ibada maalum ya
kumtambulisha Askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi
wake Himid Saga mbele ya waumini wa kanisa hilo Usharika wa Kanisa
kuu, kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa umemalizika kwa amani
na utulivu mwingi na kupelekea heshima kubwa kwa dayosisi ya Iringa
na Tanzania kwa ujumla.
"
Tumemaliza uchaguzi wetu kwa amani na utulivu mwingi na hadi sasa
hapa nimepokea salamu za pongezi kutoka Dayosisi mbali mbali na
hata nje ya Tanzania wakipongeza kwa jambo hilo kufanyika pasipo
kuwepo kwa vurugu zozote ....hii ni heshima kuwa imewekwa na yote
haya yamewezekana kutokana na kazi nzuri ya waumini kufanya maombi "
Alisema
kuwa hakuna jambo lolote alilolifanya vema pasipo kumtanguliza
roho mtakatifu hivyo ombi lake kwa wale waliopewa kazi na Mungu
ya kuongoza dayosisi hiyo ni kuepuka kusikiliza maneno ya watu
wanayoyasema barabarani na badala yake kumtanguliza Mungu na
kusikiliza kile kinachosemwa na viongozi wa dayosisi kwani maneno
ya mitaani ni ya hivyo hivyo.
"
Mimi yamesemwa mengi ila nawasamehe bure wale wote waliosema ila
nawaomba baadae wote wakatubu wapo ambao walikuwa wakifanya kazi
ya kunichafua katika vyombo vya habari na mitaani kwa kusema mambo
ya aibu dhidi yangu ila kiuharisia sivyo hivyo ....kuna wengine ni
maaskofu walipata kutamka kuwa mimi natumia vibaya fedha za chuo
kikuu cha Iringa wakati wao ni wasomi na wanajua kabisa kuwa
chuo kinakaguliwa na kuna taratibu nzuri tu za kifedha ila kwa
kuwa walikuwa wanafanya hivyo kwa kufurahisha nafsi zao na kupotosha
nasema ni wakati wa wote kutubu na wakitubu waje kuniomba msamaha "
Akifafanua
juu ya ajenda ya waumini wa Kanisa hilo jimbo la Mufindi kutaka
kuhama Dayosisi yao ya Kusini na kuhamia Dayosisi ya Iringa
alisema kuwa kuwa ajenda hiyo ilizungumzwa na aliyewasilisha
ajenda kwenye mkutano mkuu huo alikuwa ni yeye mwenyewe.
"
wapo watu wanapotosha kuwa ajenda ya Mufindi kuhamia Dayosisi ya
Iringa hakuzungumzwa kwenye mkutano mkuu nawaambia kuwa ajenda
hiyo imezungumza na mimi ndie niliyeiwasilisha usiku wa octoba 6
mbele ya wajumbe kwa kutoa maelezo maana ajenda ya askofu ni
ajenda ya mkutano mkuu hivyo sikuipeleka Halmashauri kuu wala
kamati ya utendaji nilitoa taarifa kwenye mkutano huo kuwa
Mufindi wameamua kuhamia Iringa tulipowauliza kuwa wanataka
dayosisi walisema hapana wao wameamua kuhamia Dayosisi ya Iringa
hivyo niliwaambia wajumbe kuwa hamuwezi ninyi kuwaambia wasihamie
maana dayosisi ni mali ya Mungu si mali ya mwanadamu na wakihamia
kuhamia popote wao wanaweza hivyo wajumbe wa mkutano huo
walikubali kuwapokea ..... hoja ya pili wajumbe walisema kutokana
na jambo hilo kuwa bado linasumbua kanisa waliniomba mimi
Mdegela kuendelea kuliratibu jambo hilo hadi mwisho ila kuna
uzushi umetokea kuwa katibu mkuu anasema ajenda hiyo haikuwepo ni
kweli kabisa ajenda kubwa ilikuwa ni uchaguzi mkuu lakini ile
nilisimama nikasema kama mimi kwa hiyo mimi nawajibika kusema mbele
ya wajumbe na pia nawajibika kubaki na majibu ya ule mkutano mkuu
yanayosema maamuzi ya waumini wa Mufindi ndio tutakaouheshimu ndio
kauli ya mkutano mkuu "
Askofu
Dkt Mdegela alisema kuwa watu wanasema kuwa msemaji wa dayosisi
ya Iringa ni katibu mkuu wapo hao ni wapotoshaji na wanapaswa
kupuuzwa kwani hadi sasa yeye Askofu ni msemaji mkuu wa dayosisi
ya Iringa hadi hapo januari mwakani siku ambayo askofu mpya
atasimikwa rasmi japo katibu mkuu anapaswa kusema kwa ruksa
kutoka kwake hivyo anawataka waumini wa jimbo la Mafinga kupokea
majibu ya maombi yao kuwa yamepokelewa rasmi.
Alisema kuwa waumini wa Mufindi waliomba kuhamia dayosisi ya Iringa
baada ya kudai kuwa hawapendi kuendelea kubaki dayosisi ya kusini na
hivyo walikuwa njia panda kwanza iwapo wangekataliwa Irinda
walipanga kuanzisha kanisa lao ama kuanzisha dayosisi yao lakini si
kubaki dayosisi ya Kusini.
"
Mimi ni mtaalam wa Imani hivyo niliwajibu kwa barua kuwa cha kwanza
kuwapatanisha na katibu mkuu na askofu wa dayosisi ya kusini pia
kuombana msamaha pale walipokosana ......mimi sina chuki hata
kidogo na askofu mwenzangu wa kusini Mengele amekuwa ni rafiki
yangu siku zote walipokosana wakristo wa Mufindi na askofu wao
Mengele ni pale walipokamatwa na kuwekwa mahabusu kijiji cha Mdandu
na kunyimwa dhamana na kukosa kushiriki mkutano mkuu ambayo ni
mamlaka kuu ya dayosisi na Halmashauri kubaki kimya juu ya suala
hilo sasa mimi nasimamia ukweli kuwa mimi kama askofu sikutumwa
kufunga watu polisi nimetumwa kuwakomboa wakristo ndio wanaochagua
viongozi na wanayohaki ya kusikilizwa sio kufungwa gerezani sasa
kama haya yanamkwaza mwenzangu sina jinsi huu ndio ukweli lakini
tujiulize kama Yesu angewakuta pale mahabusu mdandu angefanya nini "
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni