Na Mahmoud Ahmad Arusha,
Mahakama ya
hakimu mkazi Arusha imemwachia huru mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha
Maendeleo ya Jamii Tengeru(CDTI),Allan Mbando baada ya kumwona hana hatia
katika kesi ya tuhuma za kufanya uchochezi
kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Mbando,alikamatwa hivi
karibuni na jeshi la polisi mkoani Arusha na kisha kufikishwa mbele ya mahakama
hiyo kwa kosa la kusambaza ujumbe kupitia Facebook uliosema kuwa”Mwamunyange
pindua nchi haiwezekani wote wawe nje ,halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti”.
Akitoa hukumu hiyo jana
hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Augustine
Rwizile alisema kuwa mahakama imemwachia huru mtuhumiwa huyo baada ya upande wa
mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka yoyote.
Hakimu alisema licha ya
kumwachia huru,upande ambao haujaridhika unaweza kukata rufaa.
Mbele ya pande zote
hakimu huyo alisema kwamba mahakama imemwachia huru mtuhumiwa huyo kwa kuwa ushahidi
uliowasilishwa na upande wa jamhuri hautoshi kumtia hatiani mtuhumiwa huyo na pia
hakuna jambo lolote lenye nia ovu katika ujumbe uliosambazwa na mtuhumiwa kwa
lengo la kufanya uchochezi.
Hakimu Rwizile alisema
kwamba ujumbe uliosambazwa na mtuhumiwa huo haukuwa na umuhimu wowote kwa kuwa
haujaelezea Mwamunyange ni nani lakini pia haujataja nchi husika ambayo
ililengwa kupinduliwa.
Hakimu huyo aliiambia
mahakama hiyo ya kwamba mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili
wa kujitegemea mkoani hapa ,Moses Mahuna ameachiwa huru
na mahakama hiyo kwa kuwa ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama hauthibitishi
ujumbe uliosambazwa mitandaoni ulitoka kwa mtuhumiwa huyo.
“Kwanza ujumbe hauonyeshi
ni nani huyo Mwamunyange,pili haujataja nchi inayodaiwa kutaka kupinduliwa
lakini tatu ujumbe hauonyeshi jambo lolote la msingi lenye mahusiano ya kisiasa katika taifa linalodaiwa
kupotoshwa”alisema hakimu huyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni