Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wa watendaji wa
wilaya ya Ikungi mkoani Singida mara tu alipowasili kijiji cha Puma
kukagua mradi wa ufugaji kuku wa kusaidia watu wanaoishi na VVU
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia
TACAIDS. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo
(UNDP), Bw.Alvaro Rodriguez ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka
mazingira yanayofanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu.
Mratibu huyo alitoa wito huo wakati
alipofanya ziara ya siku mbili mkoani Singida kukagua miradi
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Baada ya kuona mafanikio katika miradi
hiyo Bw. Rodriguez, alisifu pia jamii ya Singida kwa kujitoa kuhakikisha
kwamba wanafanikisha miradi hiyo kwa kuifanya kuwa miradi yao.
Katika ziara hiyo ambapo pia Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dk. Parseko Kone na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha
ushirikiano wa kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah
Hassan walikuwepo, Mratibu alitembelea kituo cha watu wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi; Kituo cha kutibu kipindupindu na Ushirika wa
wajasiriamali vijana.
Miradi hiyo inafadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Afya Duniani (WHO),
Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kupambana na Ukimwi (UNAIDS).
UNAIDS ni mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mashirika ya TACAIDS na ZAC.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko
Kone akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada
ya kuwasili kwenye kijiji cha Puma kukagua mradi wa kikundi cha ufugaji
kuku kwa watu wanaoishi na VVU.
Mashirika ya TACAIDS na ZAC yanatambulika kitaifa na kimataifa kutokana na shughuli zake za kuhudumia umma wa Tanzania.
Miradi hiyo imewezesha vijana wengi kuwa wajasiriamali, kudhibiti Kipindupindu na kuongeza uelewa wa UKIMWI.
Alisema kwamba maendeleo endelevu
yanahusisha serikali na jamii kuangalia changamoto zinazokabili jamii na
kuzitafutia ufumbuzi kwa kuoanisha na malengo ya maendeleo endelevu
SDGs.
Miradi hiyo iliyopo Singida inatekelezwa chini ya mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa
yakifanywa shughuli mbalimbali za kusaidia wananchi wa Tanzania waume,
wake na watoto kupitia mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa
Mataifa,(UNDAP) wa mwaka 2011-2016.
Naye Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Kone
akisisitiza umuhimu wa wananchi kujimilikisha miradi hiyo, amewaambia
Umoja wa Mataifa kwamba kwamba wananchi wa mkoa huo wataendelea
kujimilikisha miradi hiyo na kuifanya ya kwao ili kuharakisha maendeleo
endelevu.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani
Singida, Chigulu Charles (wa kwanza kulia) akitoa taarifa yake ya
mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa
wa UKIMWI wilayani humo. Wa tatu kushoto,ni Mratibu mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Singida,
Dk.Parseko Kone.
Alisema maelfu ya wananchi wa Singida
wamenufaika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa
kupitia mashirika yake yaliyopo hapa nchini .
Aidha alitaka Mashirika hayo kuendelea
kusaidia miradi mbalimbali na hasa wakati Mpango wa pili wa Msaada wa
maendeleo (UNDAP II) unapokaribia kuanza mwakani, sanjari na mpango wa
maendeleo wa taifa Julai 2016.
Alisema Singida imesonga mbele katika
maendeleo katika siku za karibuni lakini bado inahitaji msaada wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuhifadhi mafanikio na
kuyaboresha.
Mhudumu wa watu wanaoishi na VVU kata
ya Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, Kelvin Mwiru, akitoa taarifa
yake juu ya majukumu ya kuhudumia watu 150 wanaoishi na VVU katika
vijiji vya kata ya Puma na vijijini jirani.Mhudumu huyo ameiomba
halmashauri ya wilaya ya Ikungi na wadau wengine kumtambua na kumpa
ushirikiano katika kazi hiyo ngumu ya kujitolea kuwahudumia watu
wanaoishi na VVU ambao wanaongezeka kila kukicha.
Mratibu mkzi wa mashirka ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (anayengalia kamera) akitoa nasaha zake mbele ya kikundi cha
ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU na wananchi kwa ujumla
wa kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi.Mwenye suti ya bluu, ni Mkuu wa
mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone wakiangalia baadhi ya kuku
wa mayai walipotembelea kikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu
wanaoishi na VVU na wananchi kwa ujumla wa kijiji cha Puma wilaya ya
Ikungi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kulia) pamoja na
Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan
(katikati) wakitazama mayai yanayototolewa na kuku hao.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone, Mkuu wa wilaya ya Ikungi,
Chigulu Charles (kulia), Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Maulidah Hassan na Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala
Fedes katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakikundi cha ufugaji kuku
cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akiondoka katika kijiji cha Puma kuelekea kijiji cha Mandewa kilichopo Singida mjini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akisalimiana na Mganga mfawidhi wa manispaa ya Singida, Dk. John
Mwombeki baada ya kuwasili kwenye kambi ya muda ya wagonjwa wa
Kipindupindu iliyopo katika kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa
Singida akiwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akiingia kwenye kambi ya muda ya wagonjwa wa kipindupindu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akisaini kitabu cha wageni katika kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akiwaeleza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone
(kushoto) na Afisa kutoka Shirika la Afya (WHO) kanda ya Dodoma, Dk.
Cyrialis Mutabuzi (kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano
wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko
Kone akizungumza na mgonjwa wa kipindupindu kutoka kijiji cha Mtavila
wilaya ya Ikungi, Jumanne Shaban. Dkt. Kone amemuagiza akirudi kijijini
akawe Balozi mzuri wa mapambano dhidi ya kipindupindu.WHO inasaidia uendeshaji wa vituo hivi pamoja na tiba.Kwa matukio ya picha zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni