Meneja
Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga, Diana Malambugi (kulia)
akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifanya usafi katika
Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo leo, kuadhimisha Siku ya
Uhuru iliyodhimishwa kwa watanzania wote kujishughulisha na shuhuli za
usafi wa mazingira.
Meneja
Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga, Diana Malambugi (kushoto)
akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Mwenyekiti wa Soko Kuu la Mji wa
Tanga la Ngamiani, Abubakar Shauri, baada ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo kufanya shughuli za usafi sokoni hapo leo, kuadhimisha Siku ya
Uhuru ambayo watanzania nchini kote walijishughulisha na kazi za usafi
wa mazingira.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, wakifanya usafi katika Soko
Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo jana kuadhimisha Siku ya
Uhuru ambayo watanzania nchini kote walijishughulisha na kazi za usafi
wa mazingira.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya Tanga Cement waliokwenda kufanya usafi
katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani, wakilisukuma trekta la
kubeba takataka ili dereva wa gari hilo aweze kuliwasha na kuendelea na
majukumu yake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanga Cement wakifanya usafi katika soko la Ngamiani mjini Tanga leo.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakiendelea na shughuli ya usafi katika soko la Ngamiani mjini Tanga leo.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Saruji Tanga wakipiga picha na baadhi ya watendaji wa
Soko Kuu la Ngamiani mjini Tanga wakati wafanyakazi hao walipokwenda
kufanya shughuli za usafi kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli kwa
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru yatumike kwa shughuli za usafi wa
mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni