MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MAULID DAR

 Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.








WATOTO WA WAHADHIRI WA UDSM WAJUMUIKA PAMOJA KWENYE 'GET TOGETHER' YA NGUVU

Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu. Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha maana watu walikuwa wanakumbushana mambo ya miaka ya 90 kwani kipindi hicho walikuwa wadogo.
Watoto wakiendelea kucheza wakati wa party ya watoto walioishi chuoni hapo kipindi wazazi wao bado ni waalimu katika chuo cha UDSM
Full Happy kwa kila tu aliyefika katika Party hiyo.
Watoto wa wahadhiri wa UDSM wakibadilishana mawazo kwenye party ya kuwaunganisha pamoja kama wanafamilia wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Hakika watoto walikuwa waki-enjoy vya kutosha maana hakuna aliyeboreka kwani kulikuwa na kila aina ya michezo kwa watoto wa rika zote.

Baadhi ya watoto wakiwa wametokelezea kwenye ukodak.

Baadhi ya watoto walioishi Chuoni UDSM wakiangalia vitabu pamoja na kununua vitabu hii ikiwa ni kundeleza utamaduni wa kujisomea.
Hakika ilikuwa shangwe kwa watoto walioishi chuoni hapo wakati wazazi wao ni wahadhiri chuoni hapo
Hivi ni Baadhi ya vitabu vilivyokuwa vinauzwa wakati wa Party hiyo iliyofanyika chuoni hapo.
Muda wa kuserebuka ulifika sasa kila mtu akaanza kuonesha umahiri wake kwenye kulisakata Rhumba.
Watoto wa Chuo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza party yao.

WACHIMBAJI WADOGO KUANDAMANA





Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Charles Mlay akizungumza juzi kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo Marema kuhusiana na maandamano ya amani kupinga migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.
WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wanatarajia kuandamana hadi kwa mkuu wa mkoa huo, wakipinga kusimamishwa kazi migodi yao 19 inayopakana na TanzaniteOne.

Wachimbaji hao wanatarajia kuandamana kwa amani mapema mwezi ujao na watamuandikia barua mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera ili ayapokee maandamano hayo wakipinga kunyanyaswa na kusimamishwa migodi yao 19.

Mmoja kati ya wachimbaji hao Charles Mlay akizungumza juzi kwenye mkutano wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Marema, alisema wachimbaji wamekuwa wananyimwa haki zao bila sababu ya msingi.

“Hakuna mtu aliye juu ya sheria kila wakati wachimbaji wadogo wananyanyasika kwa kunyimwa haki zao wakati wanachimba kihalali hivyo ni bora kufanya maandamano ya amani yatakayoeleza hisia zetu,” alisema Mlay.

Makamu Mwenyekiti wa Marema Wariamangi Sumari alisema maandamano hayo ya amani yatajumuisha wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wakazi wote wa Mirerani kwani maisha yao yanategemea madini ya Tanzanite.

“Maandamano hayo yatakuwa ya halali kabisa kwani tutaomba kibali kwa mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) na kumtaarifu mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa aje hapa Mirerani kwa ajili ya kupokea maandamano hayo,” alisema Sumari.

Omary Mandari alisema kitendo cha migodi hiyo 19 kusimamishwa kufanya kazi kimewaathiri watu wengi kiuchumi, kwani familia nyingi za wachimbaji hao zinategemea kuishi ila kutokana na hali hiyo, sasa wanaishi kwa wakati mgumu.

“Tutaandamana kwa amani kuanzia shamba la Maro na kuzungukia kwenye baadhi ya barabara za Mirerani hadi getini mnadani, kwa lengo la kuonyesha ulimwengu kuwa tunapinga migodi yetu 19 kusimamishwa,” alisema Mandari.

Naye, katibu wa Marema Abubakari Madiwa alisema azimio hilo la kuandamana kwa wachimbaji hao wadogo linaandaliwa ipasavyo ikiwemo kamati ndogo itakayoratibu mpango wote hadi kufanikisha maandamano hayo ya amani.

Zephania Joseph alisema haki ya wachimbaji wadogo haiombwi inadaiwa, hivyo huu ni wakati muafaka wa kuungana kwa wachimbaji hao kufanya maandamano ya amani ili kufikisha kilio cha kwa migodi yao 19 kusimamishwa.

LUCIAN NA FABIAN JOSEPH WATAMBA ARUSHA TOURISM MARATHON



  afisa utalii wa tanapa fredy shirima akiwa
anamkabidhi  zawadi  Mwanariadha Reginal Lucian baada  ya kushinda
kilometa 42,baada ya kukimbia kwa muda wa

1:00:05

baadhi ya wanariadha walifanikiwa kupata zawadi katika shindano Arusha tourism Marathon wakiwa katika picha ya pamoja
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanariadha Reginal Lucian  alifanikiwa kushinda kwa upande wa
wanaume,katika shindano la Arusha Tourism Marathon baada ya  kutumia
muda wa 1:00:05,akifatiliwa na mwanariadha wa kimataifa, Fabian Joseph
1:00:14, nafasi ya tatu,Gabriel Gerald muda wa 1.00.37.

katika mashindano hayo ya kilomita 42, yaliyoandaliwa na taasisi la
Alfredo Shahanga na  Mwanariadha kutoka Kenya, Evance Kiblanget
alishika nafasi ya nne baada ya kutumia muda wa 1:07 huku nafasi ya
tano ikishinda  Wilbart Peter na nafasi ya sita akishinda mwanariadha
wa kimataifa Dockson Marwa.

Kwa upande wa wasichana  Angelina Tsere alishinda kwa kutumia musa wa
1:11:17, akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa  Mary Naali muda wa
1:11:23, nafasi ya tatu ulikwenda kwa Mkenya  Ladis Shemayo aliyetumia
muda wa 1:11:37 .

Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa ni ,Afisa Michezo
wa Mkoa wa Arusha,Mwamvita Okeng'o mshindi wa kwanza hadi wa 10
walipewa zawadi.

Viongozi wengine waliotoa zawadi ni pamoja na Katibu Mkuu wa kamati ya
Olimpic Tanzania(TOC), Filbert Bayi, Rais wa zamani wa chama cha
riadha nchini(TAAA)  Franis John na Afisa  Utalii wa TANAPA Fred
Shirika.

Katika mashindano hayo, washindi wa kwanza walipoewa zawadi ta
shilingi 500,000, washindi wa pili, 250,000,washindi wa tatu, 200,000,
wanne 150,000 na wa tano 100,000 ambapo wa 6 hadi 10 pia walipewa
zawadi.

Wakizungumza wakati wa kutoa zawadi, Bayi na Okeng'o walipongeza
wanariadha waliojitokeza kwa kuonesha upinzani mkubwa na kutoa wito
mashindano haya yafanyike kila mwaka ili kusaidia kukuza utalii wa
ndani.

Mkurugenzi wa Alfredo Shahanga kwa upande wake, alisema lengo la
mashindano hayo lilikuwa ni kuhamasisha utalii wa ndani, kuhamasisha
amani mkoa wa Arusha na kutaka sasa riadha itumike kutangaza utalii.

Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya mashindano ya Arusha Tourism
Festival ni mara ya kwanza kufanyika nchini, yalidhamiwa na shirika la
hifadhi za Taifa(TANAPA), kampuni ya vinywaji ya SBC(T) Ltd,radio
Sunrise,BiG Expedetion,Mega Trade Investment,Tanzania Breweris na
Criative Solution.

MUUAJI WA AFISA WA INTELIJENSIA WA TANAPA AKAMATWA

 
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Ismail Swalehe Sang’wa (20) ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Sepuka wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida kwa tuhuma za  kumuua Afisa wa Intelijensia wa TANAPA  aitwaye Emily Kisamo (52).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo la mauaji ya Afisa huyo wa TANAPA lilitokea tarehe 18.12.2015 muda kati ya saa 2:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi mtaa uitwao Corridor Area Uzunguni jijini hapa.

Kamanda Sabas alisema kwamba, siku ya tukio hilo marehemu alikuwa nyumbani kwake sebuleni akiwa anakunywa uji ndipo mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wake wa ndani na alimvizia na kumkata shingo na kitu kinachoaminika kuwa ni panga na kisha kuchukua mwili wake na kuuweka kwenye gari la marehemu aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY.

“Baada ya kuuweka mwili wa marehemu kwenye buti alilisafisha gari hilo kwa nje na kisha kuliendesha mpaka eneo la kikwakwaru “B” kata ya Lemara ambapo alilitelekeza hapo na kisha yeye kuondoka”. Alifafanua Kamanda Sabas.

“Mara baada ya gari hilo kukaa mpaka saa 2:00 usiku ndipo baadhi ya wananchi wa eneo hilo walitoa taarifa kwetu ambapo askari wa doria walikwenda na kulichukua gari hilo kwa kulivuta mpaka kituoni. Kwa kuwa mke wa marehemu aitwaye Caroline Lukumay (38) alikuwa anamtafuta mume wake kwa njia ya simu bila mafanikio ndipo alipoamua kuja kituoni kutoa taarifa ambapo tulimuonyesha gari lililotelekezwa ambalo alillitambua mara moja”. Alisema Kamanda Sabas.

Aliongeza kwa kusema kwamba askari walimuomba mke wa marehemu funguo za akiba za gari hilo ambapo baada ya kulifungua ndipo walipouona mwili wa marehemu kwenye buti akiwa na vitu mbalimbali kama vile simu mbili aina ya Sony na Panasonic, pesa taslimu Tsh 300,000, Laptop aina ya Asus na kadi za benki tofauti tofauti.

Mara baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa alikiri kuhusika na mauaji hayo na kusema siku hiyo walikuwa wawili tu yaani yeye na mrehemu na alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa na tamaa za fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya nyumba hiyo kiasi cha Tsh. Mil.5.

Upekuzi zaidi wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwepo kwa fedha taslimu Tsh. 4,294,000, simu tatu aina ya Sumsang na vocha za mtandao wa vodacom za sh. Elfu tano tano zenye thamani ya Tsh. 70,000 ambapo vyote vilifukiwa kwenye banda la kuku.

Mbali na vitu hivyo pia mtuhumiwa Ismail Swalehe Sang’wa aliweza kuonyesha panga lenye damu ambalo alilihifadhi stoo pamoja na taulo nne kubwa, kitambaa cha mezani na suruali yake ambazo zilikuwa na damu na alizitumia yeye mwenyewe kupigia deki sebuleni baada ya tukio na kisha kuzificha kwenye migomba karibu na mabanda ya kuku.

Kamanda Sabas alimalizia kwa kusema kwamba Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watatu wengine mbali na Ismail Swalehe Sang’wa akiwemo mke wa marehemu, rafiki wa mke wa marehemu ambaye ni mwanamke na dereva wa nyumbani  wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Pichani chini gari aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY lililokutwa na mwili wa marehemu Emily Kisamo ambaye ni Afisa wa Intelejensia TANAPA uliohifadhiwa kwenye buti mara baada ya kuuawa na Mfanyakazi wake wa ndani.

WAZIRI MBARAWA AANZA KAZI RASMI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akipata ufafanuzi kuhusu namna ya kuhifadhi makontena kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Aloyce Matei (kushoto), mara baada ya kukagua Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Aloyce Matei (wa tatu kushoto), huku Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Naibu wake wakikagua mtambo wa kuchunguza makontena (scanner) katika eneo la TPA.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua mtambo wa madai na malipo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania alipotembelea Mamlaka hiyo leo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka watumishi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na uharaka wenye tija ili kukudhi matarajio ya wananchi katika wizara hiyo.

Akizungumza na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kuapishwa, Profesa Mbarawa amesema kipaumbele chake kwa wafanyakazi hao ni kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kwa kuzingatia matokeo chanya kwa haraka.

 “Tuwe tayari kubadilika, tufanye kazi ya kuwahudumia watanzania kwa moyo, tuendeleze taswira nzuri ya Wizara kwani Wizara hii ina sifa nzuri tangu ilipoanza hadi sasa’, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amefafanua kuwa uwazi na uhusiano mzuri kwa wafanyakazi ni ngao kubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo kati ya watendaji na watumishi. 

Aidha, amewataka watendaji na watumishi wa Wizara hiyo  kushirikiana na kutokuwa wanyonge kutokana na mfumo wa mabadiliko ya kiutendaji wa iliyokuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwani Wizara hizo zina uhusiano mkubwa katika kumhudumia mwananchi hivyo kuungana kwake kutaleta tija na ufanisi kwa haraka.

 “Jambo la msingi ni kufuata kanuni na sheria katika utendaji wenu pamoja na kusimamia miongozo iliyopo, utendaji wenu lazima uwe na malengo yanayotekelezeka kwa haraka”, amesema Prof. Mbarawa.

Akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Waziri huyo amehimiza matumizi ya teknolojia katika huduma za bandari ili kuweza kuwahudumia wateja kwa haraka hata wakiwa mbali.
Amewataka watumishi wa bandari kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa ushindani ili kuvutia wadau wengi kupitisha mizigo yao katika bandari za Tanzania.

“Fanyeni kazi kwa maslahi ya nchi, acheni kufanya kazi kwa maslahi binafsi, tambueni Serikali na wananchi wanahitaji huduma bora zitakazokuza uchumi wa taifa kutoka katika bandari zenu”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Edwin Ngonyani amewataka watumishi wa bandari kuacha tamaa, kuishi kwa uaminifu ili kujenga taswira mpya ya taasisi hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.

Katika ziara hiyo Waziri Mbarawa na Naibu Waziri Ngonyani waliambatana na viongozi mbalimbali wa iliyokuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

AZAM FC YAILAMBA KAGERA SUGAR 2-0

 Benchi la ufundi la timu ya Azam FC.
 Benchi la ufundi la Kagera Sugar.
 Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza la timu yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex. Azam imeshinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
 Kavumbagu akichuana na beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
 Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
 Shaban Ibrahim akimshika bukta Didier Kavumbagu.
 Uniwezi.....
 Kavumbagu akimtoka Shaban Ibrahim.
 Shaban Ibrahim akienda chini.
 Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu akimtoka beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-0.
Golikipa wa Kagera Sugar, Agathony Antony akiokoa moja ya hatari langoni mwake.