Nchi ya Kenya imeshika nafasi ya
tisa kwa vitendo vya rushwa kati ya mataifa 28 katika eneo la jangwa
la Sahara, kwa mujibu wa utafiti mpya wa rushwa uliotolewa taasisi za
Transparency International pamoja na AfroBarometer.
Kwa mujibu wa utafiti huo wananchi
wengi wa Kenya ambao ni zaidi ya asilimia 60, wanaamini kuwa tatizo
la rushwa limeongezeka nchini humo katika miezi 12 iliyopita. Aidha
nchi za Madagascar, Liberia na Zimbabwe zinaongoza kwa rushwa.
Rushwa imejikita zaidi katika jeshi
la polisi, mahakamani pamoja wakati wa kutafuta nyaraka mbalimbali
kama vile vitambulisho pamoja na vibali.
Mataifa mengine yaliyohusikakatika
utafiti huo wa rushwa ni pamoja na Nigeria, Zimbabwe, Liberia, Ghana,
Benin, Sierra Leone, Uganda, Tanzania pamoja na Madagascar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni