Muonekano
wa basi la Takbiri lenye namba za usajili T 230 BRJ baada ya kupata
ajali jana saa moja na nusu usiku katika eneo la Kizonzo, Shelui mkoani
Singida.
Katika ajali hiyo watu 18 walifariki dunia na wengine 18 wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema chanzo cha ajli hiyo ni dareva wa basi hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam kuelekea Katoro, Geita kutaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari hivyo kusababisha basi hilo kugonga na lori la mizigo lenye namba T 793 CBX.
Baada ya ajali hiyo dereva wa basi alikimbia kutoka eneo la tukio, huku dereva wa lori hilo la mizigo akiwa amepata majeraha kidogo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni