WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.
Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa
majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa
akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka
Majaliwa Kassim Majaliwa.
Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania siku hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni