MMILIKI WA FACEBOOK KUGAWA HISA ASILIMIA 99 KUTOKANA NA FURAHA YA KUPATA MTOTO

Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg pamoja na mkewe Priscilla Chan wamesema watagawa hisa zao asilimia 99 kwa ajili ya kusaidia wenye mahitaji, wakati wakitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike Max.

Mark Zuckerberg ametoa tangazo hilo katika barua kwa mtoto Max aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Wamesema wanatoa hisa hizo kwa Taasisi ya Chan Zuckerberg kwa kuwa wanataka kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri kwa Max kukulia. Msaada huo kwa sasa unafikia dola bilioni 45.

Binti Max alizaliwa wiki iliyopita, hata hivyo wanandoa hao waliamua kutangaza kuwa wamepata mtoto hapo jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni