Mvua zilizoanza upya katika mji wa
Chennai kusini wa India zimesababisha mafuriko makubwa na kusababisha
ndege na treni kusitisha usafirishaji na mamia kuachwa bila umeme.
Jeshi la India limepelekwa katika
mkoa huo kuwaokoa maelfu ya watu waliokwama baada ya mvua kunyesha
kwa siku mbili.
Watu wapatao 188 wamethibitishwa
kufa kutokana na mafuriko katika jimbo la Tamil Nadu tangu mwezi
uliopita.
Wanafamilia wakimsaidia kumuokoa mwanamke mwenye ulemavu
Wananchi wakiwa kwenye boti huku polisi wakilisukuma kuwavusha kwenye mafuriko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni