Gari
iliyokuwa ikisafirisha magazeti ya Mwananchi Communications kuelekea
mkoani Mbeya na Iringa ikiwa imepata ajali Eneo la Kitonga Mkoani Iringa
leo asubuhi.
WATU
wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria
lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda
mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa.
Ajali
hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru
kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya
lori na kupelekea kifo chao.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni