mkurugenzi
wa kampuni ya Arusha Media ambaye ni mmojawapo wa waandaaji wa
tamasha hili Musa Juma katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari
kuhusiana na tamasha hilo
Akizungumzia
tamasha hilo na kutaja michezo itakayokuwepo , Mkurugenzi wa Alfredo
Shahanga Sports Promotion ,Alfredo Shahanga katika kati
baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Mratibu wa Tamasha
hilo, Andrea Ngobole katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
TAMASHA la Utalii na amani, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 22 katika jiji la Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari Golden Rose hotel , Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alisema, tamasha hilo limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media na Alfredo Shahanga Sports Promotion.
Alisema katika tamasha hilo, kutakuwa na michezo michezo mbali mbali, ikiwepo soka, mashindano ya riadha ya Tourism Marathon, maonesho ya utalii na kongamano la utalii na amani.

"kauli mbiu ya tamasha hili ni Utalii wa ndani na amani sasa tunatoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza kushiriki"alisema
Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi Alfredo Shahanga alisema, maandalizi yote muhimu yamekamilika.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wadhamini zaidi kujitokeza kudhamini ili kuhakikisha wakazi wa Arusha wanashiriki kuhamasisha utalii wa ndani na kuhubiri amani.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wadhamini zaidi kujitokeza kudhamini ili kuhakikisha wakazi wa Arusha wanashiriki kuhamasisha utalii wa ndani na kuhubiri amani.
Naye
mkurugenzi wa kampuni ya Arusha media ambaye pia ni mmoja wapo wa
waandaaji wa tamasha hilo alitaja michezo ambayo itakuwepo ni pamoja na
kukimbiza kuku,kuruka kamba,kukimbia
na magunia ,riadha ambapo alisema kuwa kutakuwa na mbio za kilometa
tano,half marathoni pamoja na full marathoni ambapo alieleza kuwa mbio
za full marathoni zenyewe zitafanyika siku december 13.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni