Afisa
Masoko wa kampuni ya simu mkoa wa Morogoro, Aminata Keita akizungumza
jambo wakati wa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye
lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na
kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16
hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Mkufunzi
kutoka Veta kanda ya mashariki na kati, Marthin Mollel akitoa mafunzo
ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu
ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu
yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika
ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Baadhi
ya vijana walioshiriki mafunzo ya ujasiliamali wakimsikiliza mkufunzi
(hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa
kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza
kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa
kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
vijana
zaidi ya 200 mjini Morogoro wamehudhuria warsha ya siku nzima ya
'Airtel FURSA Tunakuwezesha. Airtel Fursa ni mpango unaowalenga vijana
wemye umri kati ya miaka 18 -24 na wanamiliki biashara ndogo ndogo kwa
kuwapatia ujuzi na nyenzo muhimu kwa mafanikio ya biashara zao na kuweza
kujenga fursa kwa wengine.
Akizungumza
katika warsha hiyo, mmoja wa washiriki bw. Musa Ndauka alisema;"napenda
kuwashukuru Airtel kwa kutambua changamoto ambazo vijana tunakumbana
nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya
kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na
zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua
jukumu hili na kutusaidia sisi vijana wa Morogoro"
"Leo
hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa
kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi
ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko
la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja
zaidi. Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha
yangu. "aliongeza Ndauka
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo afisa masoko wa Airtel Tanzania,
Aminata Keita, alisema "tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana
wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira. Nchini
Tanzania, vijana wapatao milioni moja kila mwaka huwa wanapata matatizo
ya ajira.
Tunahitaji
kuwawezesha na kubadili mawazo ya kutaka kuajiriwa kwa kuwasaidia kuwa
wabunifu na kuweza kujiajiri. Mpaka sasa Airtel FURSA Tunakuwezesha
imewawezesha vijana zaidi ya 1200 kupitia warsha hii na tuna mpango wa
kufikia vijana wapato 2000 mwaka huu peke yake.
Tunatambua
na kuwapongeza hawa vijana ambao ni wafanyabiashara wadogo wadogo kwa
juhudi walizofanya na kuweza kufikia hapa walipo licha ya changamoto
hizi zote. Nami nawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuomba
kuwezeshwa kupitia mradi wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha”, "alisema
Keita
Alitoa
wito kwa vijana katika mkoa wa Morogoro kutumia nafasi hii ya “Airtel
FURSA Tunakuwezesha” kwa kuweza kujiendeleza kibiashara na kuhakikisha
kuwa wanapanuka kibiashara. Morogoro ina mambo mengi mazuri sana kwahiyo
vijana watumie mji wao kuweza kujiendeleza na vile vile kupanua uchumi
wa Morogoro.
Huu
sio muda wa kukaa bila kazi wakati kuna fursa inayokuwezesha kupata
maarifa ya bure. Vijana wetu lazima wajishughulishe na vitu tofauti
vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazowafanya
wafaidike na kuweza kujikomboa na umasikini, "alisema Keita
Alisisitiza
kwamba mpango wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unawalenga wale vijana
ambao tayari wanabiashara na walio katika umri kati ya miaka 18-24, na
anayeishi Tanzania na kuendesha biashara zake hapa nchini. Ili kijana
kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi
kwenda kwa namba 15626 au barua pepe kwa airtelfursa@tz.airtel.com au
kutembelea mtandao wa Airtel na kurasa za kijamii kwa maelezo zaidi.
Keita
alihitimisha kwa kusema Airtel imedhamiria kufanya kazi na Serikali ili
kusaidia kuwajenga vijana na kuwaweka kuweza kuamini kwamba Airtel FURSA
Tunakuwezesha' ipo kwa ajili yao na kuleta mabadiliko na msisimko kwa
vijana mkoani Morogoro na maeneo mengine ya hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni