Na Faustine Ruta, Bukoba.
Uwanja
wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2
Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa
muda wa siku 14 tu.
Wakaazi
wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live
bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo
inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo
ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja
vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. Uwanja huu umejengwa kwa
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.
Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.
Taswira
ya Nyasi zenyewe za Bandia zikiwa zimetandazwa katika Uwanja huo wa
Kaitaba uliopo Bukoba Mjini ambao hutumiwa na Timu ya Hapa Bukoba Kagera
Sugar ambayo kwa sasa inaendelea kutumia Viwanja vya Ugenini.
Katibu
wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi
Nchini akizungumzia swala zima la Uwanja huo wa Kaitaba na Waandishi wa
habari leo jumatatu 02 Novemba, 2015. Chama ameeleza kutokana na kasi
iliyopo na kama Mafundi hawatakwama Uwanja huo utamalizika ndani ya Wiki
mbili tuu.
Taswira kamili
Uwanja
huo umeanza kuwekwa nysi rasmi leo na ndani ya siku 14 utamalizika na
taratibu nyingine zitafuata na Timu ya Kagera itaanza kuutumia Uwanja
huo. Uwanja huu sasa utakuwa umeongezeka katika Viwanja vilivyowekwa
nyasi hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Uwanja wa Uhuru uliopo
Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani
uliopo Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni