Mwanariadha Oscar Pistorius ametiwa
hatiani kwa kosa la mauaji baada ya mahakama ya rufaa nchini Afrika
Kusini, kutengua hukumu ya awali ya kuuwa bila ya kukusudia.
Pistorius alimuua mpenzi wake
mwanamitindo Reeva Steenkamp mwezi Februari 2013, kwa kumfyatulia
risasi mara nne akiwa ndani ya choo ambacho mlango wake ulifungwa.
Kwa sasa Pistorious ambaye ni
mwanariadha mlemavu wa miguu yote miwili yupo anatumikia kifungo cha
nyumbani, baada ya kukaa jela mwaka mmoja kati ya miaka mitano
aliyohukumiwa.
Pistorius sasa atarejea mahakamani
kubadilishiwa adhabu na kuwa ya mauaji.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni