Vikosi vya jeshi la Cameroon
vimewaokoa watu 900 waliokuwa wakishikiliwa na kundi la Boko Haram,
Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo ametangaza.
Waziri huyo Joseph Beti Assomo
amesema vikosi hivyo pia vimewauwa wapiganaji wa kundi hilo 100 hadi
kufikia mwisho wa mwezi Novemba.
Hata hivyo hakuna uthibitisho huru
kuhusiana na operesheni hizo za jeshi la Cameroon katika eneo la
kando la mkoa wa Kaskazini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni