Taarifa
zilizotufikia zinasema watu kadhaa wanahofiwa kufa na wengine
kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Simba Mtoto lililokuwa linasafiri
kutoka Tanga kuelekea jijini Dar es Salaam kugongana na lori la mizigo
leo asubuhi.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinasema juhudi kubwa zinaendelea kufanywa na
jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwanasua abiria ambao bado
wamenasa ndani ya basi hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa magari hayo yaligongana uso kwa uso. Tutawaletea taarifa zaidi kadiri zitakavyotufikia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni