Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54 za madiwanikupinga
Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia
jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali.
Tume
imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea (warufani) na
Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi
rufaa za Wabunge. Leo tarehe 31/82015 zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa
38. Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya Tume na Wasimamizi wa
Uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia
maamuzi ya kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki
katika uchaguzi.
Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ni 16 na Tume imerudisha wagombea 13kati
ya hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya Wasimamizi wa
Uchaguzi. Hii ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha
makosa ya kisheria au kiufundi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni