Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Mkutano wa
Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais
Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali
hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa
kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao
unaudhuriwa na mamia ya washiriki unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha
umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya
kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katika Mkutano wa Kimataifa
wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ili aweze kuufungua mkutano huo. Katika
hotuba yake Waziri Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi umekuwa
muhimu kwani unaleta uwazi pamoja na uwajibikaji katika utoaji wa huduma.
Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika,
unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa
uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wapili kulia meza kuu, Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. Anayefuata ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni
Sefue.
Sehemu
ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika
wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa makini wakati akitoa
hotuba yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa
kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi
zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta
maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya
washiriki kutoka nchi 23 barani Afrika unalengo la kutoa elimu pamoja na
kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali
barani humo.
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akitoa hotuba yake katika Mkutano wa
Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ambao
unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa
elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika
sehemu mbalimbali barani Afrika. Wenyeji wa mkutano huo ni Serikali ya Tanzania
wakishirikiana na Benki ya Dunia.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa ameshika ndege ambayo inapaa bila rubani (Drone) na yenye
uwezo wa kuchukua matukio mbalimbali ikiwa angani, wakati alipotembelea Banda
la Buni Hub ambalo lipo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, mara
baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika
unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. Wapili kulia ni Mtaalamu wa Benki ya Dunia, Frederick Mbuya akitoa
elimu ya ndege hiyo kwa Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (kulia kwa Rais Kikwete) pamoja na viongozi wengine walioambatana na
Rais huyo.
Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni