Muonekano wa jengo la choo ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.
Muonekano wa choo ambacho
kilikuwa kikitumika awali kabla ya ujenzi wa choo kipya ambacho
kimejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Flaviana Matata Foundation, Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation,
Francesca Tettamanzi wakitoka kukagua vyoo hivyo kabla ya uzinduzi
rasmi.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Flaviana Matata Foundation katika tabasamu bashasha baada ya kukagua
vyoo ambavyo vimejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation. 
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji
Foundation, Francesca Tettamanzi kwa pamoja wakifunua kitamba kuzindua
jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa vyoo vya kisasa katika
Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Pwani.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji
Foundation, Francesca Tettamanzi wakionekana wenye nyuso za furaha baada
ya kufunua kitambaa kwenye jiwe la msingi.
Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji
Foundation, Francesca Tettamanzi akikata utepe kuzindua rasmi choo cha
kisasa katika shule ya Msingi Msinune kilichojengwa na Mo Dewji
Foundation. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo
Bagamoyo, Msami Mgoto pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakishuhudia
tukio hilo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
Taasisi ya Mo Dewji ikishirikiana na
Taasisi ya Flaviana Matata, imekabidhi choo katika Shule ya Msingi
Msinune ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani kitakachosaidia wanafunzi wa
shule hiyo.
Tukio la kukabidhi choo hicho
limefanyika katika shule hiyo mapema leo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa
Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana Matata ambapo ameelezea kuwa,
wamekua wakiwapatia wanafunzi wa Msinune vifaa vya shuleni tangu mwaka
2014 na mwanzoni mwa mwaka jana aliombwa kuwa mlezi wa Shule na kuweza
kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo suala hilo
la vyoo vya waalimu na wanafunzi, madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Flaviana amesema baada ya kuguswa
aliweza kumshirikisha Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Mohammed
Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji, alikubali kutoa msaada huo
kupitia taasisi yake hiyo ya Mo Dewji Foundation na kuweza kujenga choo
hicho chenye matundu nane.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo
ya Msinune, Bw. Msami Mgoto ameshukuru taasisi ya Mo Dewji kwa msaada
wa kufadhili ujenzi wa choo hicho huku akielezea kuwa itasaidia
wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma hapo licha ya kuwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha
Msinune, Ramadhani Mtokeni aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa niaba ya
wananchi wa kijiji cha Msinune huku akiomba iendelea kuwasaidia pindi
wanapokuwa na matatizo.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka Mo
Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi amepongeza juhudi za Flaviana
Matata za kusaidia jamii ikiwemo kukua kwa elimu hapa nchini hivyo
wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Francesca ameongeza kuwa, Mo Dewji
kupitia msaada huo, wanafunzi watakuwa katika mazingira mazuri na safi
kwa afya zao ikiwemo kusoma bila kuwa na tatizo la awali la choo, kwa
sasa na miaka ijayo choo hicho kitakuwa mkombozi na msaada mkubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni