Kaimu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza na wajumbe
wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) katika hafla fupi ya
uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika mjini Moshi. Watatu kulia meza kuu ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud
Sururu, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano.na
kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
Mkufunzi
Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Erasmi
Francis akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya Chuo
hicho, kamera inayotumika kuchukua kumbukumbu za usalama kwa ajili ya
watu wanaopita katika mipaka ya nchi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Watatu kulia ni Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
hicho, Kinemo Kihomano (Wasita kushoto)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati waliokaa), Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Victoria Lembeli (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja
na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mara baada
ya Katibu Mkuu huyo kuzindua Bodi hiyo mjini Moshi. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni