Polisi nchini Uganda imemkamata
kiongozi wa upinzani anayewania urais Dk. Kizza Besigye akiwa kwenye
moja ya barabara kuu Jijini Kampala.
Mashahidi wamesema polisi walifyatua
mabomu ya machozi kuwasambaza mamia ya wafuasi wa Dk. Besigye
waliokuwa wakimsindikiza.
Dk. Besigye ni miongoni mwa wagombea
urais saba wanaowania kumg'oa madarakani rais Yoweri Museveni ambaye
ameiongoza Uganda kwa miaka 30, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Alhamisi wiki hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni