WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAELI AANZA KUTUMIKIA ADHABU YA KIFUNGO JELA

Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli Ehud Omert ameanza adhabu ya kutumikia kifungo cha jela cha miezi 19.

Olmert alihukumiwa kifungo cha miaka sita mwaka 2014, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa wakati akiwa Meya wa Jerusalem.

Adhabu, hiyo ilipunguzwa na kuwa miezi 18 Desemba mwaka jana, na mwezi mmoja mwingine uliongezwa wiki iliyopita kwa kujaribu kuzuia haki kutendeka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni