Benki
ya NMB imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya shilingi milioni 5
kwa shule ya Msingi Mtibwa iliyo katika kata ya Turiani – Mvomelo mkoani
Morogoro. Huu ni mwendelezo wa benki kujali wateja na jamii
inayozunguka matawi yake huku ikiamini kuwa ni kupitia jamii ndipo
wateja wake wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa
jamii ni utamaduni waliojiwekea.
Kwa
mwaka huu – 2016 NMB imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1
kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na afya pamoja na kusaidia
vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwenye elimu ikiwa ni pamoja na
Tehama na maabara kwa shule za msingi na sekondari.
Meneja
wa Tawi la NMB Turiani akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Shule ya Msingi
Mtibwa - Enock Kagonji huku Mwanafunzi wa darasa la sita Nasma Seif
akishuhudia tukio hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakiwa wamekalia madawati waliyopewa na NMB
Meneja
wa NMB Kanda ya Mashariki – Nazaret Lebbi akikata utepe kuashiria
kuanza kwa matumizi ya madawati yaliyokabidhiwa na NMB kwa shule ya
msingi mtibwa.
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AZUNGUMZIA TUKIO LA KUSHAMBULIWA HELKOPTA YA DORIA ILIYOPELEKEA KIFO CHA RUBANI WAKE.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi
wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 09/02/2016 katika ukumbi wa
Ngorongoro Makao Makuu ya Wizara hiyo kuzungungumzia tukio la hivi
karibuni (tarehe 29 Januari 2016) la kushambuliwa kwa helkopta ya doria
na kuuawa Rubani Rogers Gowel Raia wa Uingereza. Katikati ni Naibu
Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Wizara hiyo
Maja Gen. Gaudence Milanzi. SOMA TAARIFA KAMILI HAPO CHINI (SCROL DOWN
FOR MORE DETAILS)
Mkutano na Waandishi wa Habari ukiwa unaendelea.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, INSPEKTA Jenerali (IGP), Ernest Mangu, kulia akifafanua moja ya jambo katika Mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Maliasili walioshiriki mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keraryo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni