Kiongozi
Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea
michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na
Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Arch. Dudley Mawalla
(kulia) kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika
hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa
kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya
PPF, Injinia Marko Kapinga.
DG
William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha
kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti
iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha
miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji,
idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe.
Jengo
hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10
sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina
thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu
Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote
muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta
makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na
moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha
magari ndani ya jengo.
Kwa
mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch
Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018
ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica
completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo
imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika
ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya
muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka
kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na
Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa.
Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo
tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji
wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24
wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara.
Mkandarasi
Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa
huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C
(EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji
taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International
Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama
makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji
na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB.
Injinia
Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua
makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna
jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi
mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake
ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director
General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya
jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia
Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni