Safari ya mwisho ya Marehemu Clara Pius Msekwa

Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiwasili nyumbani kwa Mama yake mkubwa Kimara , Korogwe kabla ya ibada ya kumuombea marehemu na kupelekwa kuzikwa katika makaburi ya Mburahati Jijini Dar Es Salaam.
Ibada ya Kumuombea Marehemu Clara Pius Msekwa ikiendelea nyumbani Kwa mama mkubwa wa marehemu maeneo ya Kimara Korogwe kabla ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Mburahati jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mfanyakazi wa Proin Group, Emmanuel Mdinka akipita pembeni ya jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa Kwaajili ya kutoa heshima zake za mwisho kabla ya kupelekwa kupumzishwa katika nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Mburahati. 
Waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu Clara Pius Msekwa wakitoa heshima zao za mwisho
 
Mama mkubwa wa marehemu Clara Pius Msekwa akilia kwa uchungu mara baada ya kutoka kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Clara Pius Msekwa
Ndugu, jamaa, marafiki na waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu wakitoka kutoa heshima zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa ambae alikua mfanyakazi wa Kampuni ya Proin Group Limited.
Baadhi ya wafanyakazi wenzie na marehemu Clara Pius Msekwa wakiwa na majonzi ya kuondokewa na Mfanyakazi mwenzao
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiwasili katika Makaburi ya Mburahati tayari kwa kumpumzisha Marehemu Clara Pius Msekwa.
Sala ya kumuombea Marehemu Clara Pius Msekwa kabla ya kuzikwa ikiendelea
Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiingizwa katika kaburi tayari kwa kuzikwa.
 Ndugu, marafiki pamoja na waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu Clara Pius Msekwa wakiweka mashada ya maua juu ya kaburi ya marehemu Clara Pius Msekwa katika makaburi ya Mburahati.
Marehemu Clara Pius Msekwa alifariki dunia mnamo tarehe 11-02-2016 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mara baada ya kuugua kwa muda, Marehemu Clara alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kujaa maji hali iliyopelekea kuteseka kwa muda akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mpaka hapo mauti yalipomfika.
Marehemu Clara Pius Msekwa alikua mfanyakazi wa kampuni ya Proin Group limited ambapo aliwahi pia kufanya kazi katika kampuni ya Zantel na kabla aliwahi kuwa mwalimu wa shule ya awali. 
Kampuni ya Proin group inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote walioweza kushirikiana katika kuokoa maisha yake tokea alipokuwa mgonjwa lakini kwa bahati Mungu ameweza kumchukua Mja wake. 
Vilevile Proin inapenda kuwashukuru wale wote walioshirikiana nao katika msiba huu mzito ulioikimba familia yake, ofisi yake na hata marafiki zake kwa kuweza kuwa sehemu ya faraja kwetu.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Clara Pius Msekwa mahala pema peponi Amen

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni