TRENI MBILI ZAGONGANA UJERUMANI NA KUUWA WATU WANNE

Treni mbili za abiria zimegongana Ujerumani katika jimbo la Bavaria, polisi wamesema watu wanne wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea huko Bad Aibling mji ambao upo umbali wa kilomita 60 kusini mashariki mwa Munich.

Moja ya treni ilitoka nje ya reli katika ajali hiyo ambayo imepelekea mabehewa kadhaa kupinduka.
                                 Majeruhi akichukuliwa kwa helkopta kupelekwa hospitali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni