POLISI WAPAMBANA NA WAUZA VYAKULA HUKO HONG KONG

Mapigano yametokea Hong Kong katika wilaya ya Mong Kok wakati polisi wakifunga vibanda haramu vya kuuzia chakula vilivyojenga kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya wa Lunar.

Ghasi ziliibuka usiku wakati wakaguzi wa chakula na afya wakijaribu kuwaondoa wachuuzi wa vyakula kwenye makutano ya Mtaa wa Portland na Shan Tung.

Watu wenye hasira wamewarushia polisi vipande vya matofali pamoja na vitu vingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni