Mcheza kamari mmoja anayedaiwa kuwa
ni raia wa Tanzania amepandwa na hasira na kuwakata kwa panga
mameneja wawili wa Casino baada ya kucheza kamari na kuliwa shilingi
30,000 za Kenya huko Eastleigh, Nairobi.
Mcheza kamari huyo John Muchanga
hata hivyo alidhibitiwa na kisha kuuwawa na watu wenye hasira
alipokuwa akijaribu kumshambulia meneja wa tatu kwenye casino ya City
View iliyopo barabara ya Tenth.
Mkuu wa polisi Jijini Nairobi
Japheth Koome amesema Muchanga alimfuata meneja mwanamke akimtaka
amkopeshe fedha za kucheza kamari baada ya kuliwa na aliponyimwa
alitoka nje na kuja na panga na kuanza kumshambulia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni